Caleb Onyo

Mtume Nabii Elisheva Eliyahu Kiongozi wa pekee wa Huduma ya AMIGHTYWIND kwa wakati huu.

VIONGOZI WAKUU WA HUDUMA HII NI YAHUVEH, YAHUSHUA, NA RUACH HA KODESH.

Mtume Nabii Elisheva Eliyahu amekuwa Mzalishaji na Kiongozi wa Huduma ya AMIGHTYWIND kwa muda wa miaka 25! Mnaweza kuniandikia mkitumia fomu ya mawasiliano.

TAREHE APRILI 4 2019 HUDUMA YA AMIGHTYWIND ITAKUWA NA MIAKA 25 NA PIA NI SIKU YA KUZALIWA KWAKE MTUME NABII ELISHEVA ELIYAHU.

MHUDUMU (KUAMULIWA NA YAHUSHUA BAADA YA KUUNGAMA, KUTUBU KWA KWELI, UKOMBOZI NA MAAMUZI YAKE EZRA CALEB. TAREHE 2/24/2019 YAHUVEH NA YAHUSHUA WALIAMURU ELISHEVA KUFANYA HAYA KAMA ALIPOKUWA KATIKA MAOMBI.)

Ninataka watu wajue kuwa katika mwaka wa 2016 na 2017 Ezra Caleb alitumiwa na YAH kuwa Baraka kuu kwa huduma hii na tulihudumu pamoja.

Tafadhali bonyeza picha iliyoko chini kutazama video “Mfupa Wa Mfupa Wangu, Mwili wa Mwili Wangu”

Shairi ya “Mfupa Wa Mfupa Wangu, Mwili wa Mwili Wangu”

YAHUSHUA Aliniambia niongezee ujumbe huu Tarehe Machi 7, 2019. Ilikuwa miaka tatu iliyopita leo Ezra Caleb alipokuja ndani ya maisha yangu na huduma hii. Ezra Caleb alisema kuwa aliposoma shairi hii ya mfupa wa mfupa wangu, mwili wa mwili wangu , sote tulijua kuwa ni yeye YAH Alitabiri juu yake mwaka wa 1997. Mojawapo ya vitu anavyopenda kufanya, na mimi pia, ilikuwa kusoma shairi hii ya kinabii. Alikuwa anaziweka jina zetu ndani yake.

Hii ni kutoka Unabii 139:

Shairi hii ni Unabii na ni ahadi kwa dada zangu katika YAHUSHUA – wale ingawa walipeana akili, mwili, roho, na nafsi zao kwa YAHUSHUA, bado wamewekwa mateka kwa ndoa mbaya au wamewekwa mateka na fikra za ndoa mbaya zilizotoka jehanamu. Ni YAHUSHUA pekee Anayeweza kukuachilia huru kwa wale wanaokuumiza au waliokupiga vidonda vikuu kwa akili, mwili, roho na nafsi yako. Hii ni ahadi yako na ahadi yangu, kwamba mahali umejua mabaya utajua mazuri.

Niliamka MUNGU YAHUVEH Akiyazungumza Maneno haya kwangu, “Nilikutumia Mchungaji Harry Regan. Kwa misimu minne utajua kama thibitisho. Alifunga ili uweze kusikia…”

MUNGU Aliniambia “Amka na uyaandike chini.” BABA YAHUVEH Alinipa shairi hii kuiandika, na MUNGU Alipokuwa Anazungumza kwa ndoto, Akiniamsha na Maneno haya ya shairi ifuatayo. Nilidhani haya Maneno ni ahadi kwangu mimi. Sasa ninajua haya ni ya dada zangu WOTE, katika (YAHUSHUA MASIHI wetu), waliotembea njia sawa kama niliyoitembea.

Hii ni ahadi iliyopewa kwangu na MUNGU, na sasa ninaitoa kwa wale wanaongoja mazuri katika bwana aliyekadiriwa na MUNGU, ambapo walijua mabaya zaidi kutoka jehanamu. Soma haya na dai haya kama ahadi yako.

Wanaume ambao waliokadiriwa kwa wanawake hawa jueni haya: mna mwanamke ajaye aliyepitia tanuu ya moto na kutoka safi kushinda dhahabu. Atakujali kwa njia ambayo mwanamke ambaye hajawahi kuteseka kwa njia ambazo sisi tumepitia, atamjali bwana mtakatifu. Kama kuna yeyote anayetaka kuyatoa haya kwa tovuti zao niandikieni mimi na mnijulishe. Sifa, heshima na utukufu kwa YAHUVEH!

Ilikuwa msimu wa kiangazi wa 2018 ambapo shida zilianza kutokea.

Ezra Caleb, ndivyo Asemavyo YAHUVEH, ilichukua siku 6 kwa WAUMBA YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH kuumba dunia hii na bado Ezra Caleb, amehisi kutusiwa na cheo kiongozi msaidizi Nilipomuita kuhudumu kando ya Elisheva kama bwana na bibi. Kwa hivyo MIMI YAHUSHUA Nikamuamuru kuondoa jina la Ezra Caleb (kama kiongozi msaidizi) kutoka ukurasa wa mbele. Ezra Caleb wewe sio kiongozi mkuu wa Huduma hii. UONGOZI MKUU MTAKATIFU YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH HA KODESH ndio VIONGOZI WAKUU wa Huduma hii.

Kabla bibi hajanyenyekea kwa bwana yake na kumtii, lazima yeye anyenyekee kwa YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH. Ezra Caleb, umemshtaki Elisheva kwa kutonyenyekea kwako kwa sababu amekataa kukuweka wewe juu ya MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA, na RUACH HA KODESH kama mkuu wa huduma hii. Umemshtaki kwa kuwa bibi asiotii kwa kukataa kunyenyekea kwako. MIMI YAHUSHUA Ndiye bwana wake wa KWANZA na Nimeyajaribu maneno yake. Kwa kuwa nyote wawili mmezungumza mbele ya dunia kuwa hamtawahi kuweka mwingine mbele ya UTATU MTAKATIFU. Elisheva amethibitisha haya. Ingawa hataki kukukera, ananitii MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH.

Kila mtu anayesoma haya atajaribiwa kuona kama watafanya yaya haya. Kwa kuwa hamfai kupenda karama kushinda yule anayewapa karama hizo. Tetemeka ewe Ezra Caleb, Tetemeka. Kwa kuwa umefanya MIMI YAHUVEH kukasirika. Umefanya YAHUSHUA kukasirika na umefanya IMMAYAH kukasirika. Kwa kuwa Nilikupa bibi yako Elisheva kama zawadi. Nyote wawili mliitwa kufunza na kuhudumu pamoja mkihubiri wokovu na agano jipya la damu ya MWANA KONDOO MTAKATIFU WA KWELI wa YAH, YAHUSHUA MASIHI.

Tetemeka Ezra Caleb, Tetemeka. Je, zipo wapi unabii zilizofaa kutafsiriwa kwa kiebrania? Mbona ulianza kazi nzuri katika kutafsiri unabii kwa kiebrania na alafu ukaacha? Dada yako anayeishi kule Israeli alikuwa tayari kukusaidia na hajui YAHUSHUA kama unavyomjua. Upako ambao ungekuwa, kama tu ungeendelea.

Je, hautaki kuwaokoa watu wako? Watu WANGU? MIMI Ninakuaibisha? Unamuogopa binadamu kushinda MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH? Miaka hii yote Nimekungoja wewe kutafsiri Unabii ZANGU Takatifu katika Kiebrania na ziko wapi? Utafikia Israeli vipi? Unafikiria waweza kuyafanya haya pekee yako?

USIOGOPE kile ambacho binadamu anaweza kufanya kwa mwili wako na hawezi chochote kwa nafsi yako, lakini ogopa kile MIMI YAHUVEH Naweza kufanya kwa mwili wako na nafsi yako. Mbona huhubiri Wokovu? Kama vile kwa urahisi Nilivyofunga mlango huu sasa kwa kukuondoa kwa uongozi, ndivyo vile kwa urahisi Ninaweza kuufungua tena kama tu utatii. Unazungumzia kutii, lazima kwanza wewe uwe mfano Ezra Caleb. Tetemeka Ezra Caleb, O Tetemeka. Kwa kuwa utajibu kwa mengi. Wewe, na hakuna mwanamume au mwanamke mwingine hamtawahi kuwa mkuu wa Huduma hii ya Amightywind. Itakuwa kamwe UTATU MTAKATIFU. Unapoanza kufikiria haya na kujiweka kwenye kiimo, SISI UTATU MTAKATIFU TUTAKUGONGA CHINI! Utagundua kuwa SISI huwaadhibu watoto tunaowapenda.

Kwa kuwa haya hayana lolote la kufanya na upendo ulio kati yenu, linahusu upendo ambao mnayo kwa SISI, UTATU MTAKATIFU. YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH mpendwa, ROHO MTAKATIFU MPENDWA. Kwa kuwa upendo wenu kwa SISI utajaribiwa kuona kama SISI ni Kwanza katika maisha yenu na upendo, au kama sisi ni wa pili na chini.

Kwa wale mnaosoma haya, nyinyi pia mtajaribiwa kama mnatupenda SISI, UTATU MTAKATIFU na kama SISI kwa kweli ndio wa KWANZA katika maisha yenu na upendo. Tetemeka O Ezra kwa kuwa utawajibika kwa machozi yote ambayo bibi yako wa pekee Elisheva Amelia na kila kilio kilichokuja mbele ya kiti cha enzi kutoka kwa mdomo wake akiuliza Baba YAH Mbona? Unasikiza maono yanayokujaza na kiburi na ibada ya sanamu. Maono hayo yalitumwa kutoka kwa shetani, kwa kuwa hawa ni wajumbe wa shetani. Wale unaowaita watoto wako wa kiroho wako na mfano wa Utakatifu, lakini hawana Utakatifu ndani yao.

Nimemuambia Elisheva kuthibitisha haya kwa video kuwa wanaweza kubadili umbo lao. Hapo mbeleni walikuwa na wokovu wa nepi na sasa umezungukwa na malaika walioanguka unavyomkemea Elisheva kwa kukuonya, “Usiwasikize hawa wenye maono ya uongo kwa kuwa wanafanya uchawi.” Alikuonya kuwa Christina Gunther (D’vorah), Shengya Pu (Hannah), Donovan Todd (Shimshon) na wote waliokuzunguka sasa waliokuwa wakifanya. Wanakushuhudia na kukuabudu kama sanamu ya dhahabu ya ndama na SISI, UTATU MTAKATIFU TWASEMA KUWA UMETUUDHI! Kwa kuwa wathamini Unabii na wasema kuwa zilikuwa kama johari kama Elisheva alivyozungumza ulikuwa unaziandika na mkono wako ili uzisome tena baadaye.

Sasa umezungukwa na wale unaowaita watoto wako wa kiroho ambao wanafanya uchawi kwa kusudi na wamefungua jicho lao la tatu. Je, wafikiria maono haya na ndoto hizi zatoka wapi? Wafikiria ni kwa nini wanataka uamini kuwa wewe ni zaidi ya mwanamume tu aliyeokolewa na damu ya YAHUSHUA? MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH tumefunga masikio YETU kwa nyimbo ya Christina. Kwa kuwa SISI tunajua roho ya kweli iliyoko ndani ya wao wote, wanaume na wanawake ambao Elisheva alikuonya uwakimbie wakijaribu kushindana kwa kutoa maono. Haya pia yanahusu, Tatiana Harvey Williams (Bat’El) na Rickey Williams (Avi’El), Jason Benn (Avichai) na Stephen Rosii Jr (Natan’El), o mmefanya nini. Ezra Caleb unafunza kutoka kwa vitabu vya kale [vingine ni vizuri na vingine ni vibaya] badala ya maandiko yenye ushuhuda wa YAHUSHUA.

Tetemeka o Ezra Caleb kwa kuwa umefunza wanaume na wanawake, kile kikundi kidogo kinachokuzunguka kukariri maneno ya kiebrania ambayo sio chochote ila tu maneno ya kurudiarudia. Hayatoki kwenye moyo au nafsi na maneno yenu ya kiebrania haitawaleta kwa wokovu.

Hii sio hekalu ya Waebrania Halisi, ewe mwanamume wa Israeli. Kwa kuwa mna pepo ya dini, ambayo ni pepo ya mafarisayo sasa na mnaona ni heri kufunza sehemu za torati kushinda kufunza na kuwafanya wakariri maandiko ya Kiingereza kwenye agano jipya yenye ushuhuda wa YAHUSHUA.

Unamkemea Elisheva anapokuonya kuhusu macho ya tatu na umeruhusu macho ya tatu kufunguliwa kwako. Hii ndiyo sababu hauwezi tena kuwa kwenye uongozi mpaka uungame kila kitu ulichofanya kwa MIMI YAHUSHUA na bibi yako Elisheva. MIMI YAHUSHUA Ninakuita urudi KWANGU. Funza juu YANGU tena. Kumbuka ulipotoa kila kitu kwa ajili YANGU? Mali yako yote? Kumbuka Nilipokuleta kwa Elisheva Machi 7 2016? Na MIMI Ndiye Niliyekupa hamu ya mwanamke huyu mtakatifu ambaye sasa ni bibi yako na kuwa msaidizi kwa kuongoza nafsi kwa MIMI YAHUSHUA, pamoja ambapo upako hizi mbili Nikaziunganisha pamoja kuwa moja.

Tafadhali bonyeza picha iliyoko chini kuona video “Upako Mbili Zimekuwa Moja!”

Upako Mbili Zimekuwa Moja!

O mwana mpendwa MIMI YAHUSHUA Ninakuuliza, yuko wapi yule bwana mtakatifu? Yuko wapi yule mwanamume mtakatifu aliye na upako Niliyemuamuru kabla ya bibi yako Elisheva kutabiri kwa umati? Nilikufanya uwakemee maadui waliokataliwa na aina zote za wale waliokuwa wanashambulia na uchawi. Nilikupa upako wa kumlinda na ndimi takatifu na sasa umezungukwa na maadui wake na kula kwenye meza ya karamu ya ndoto zao na maono yao ambayo shetani alikutengenezea wewe ili ufeli misheni wewe na yeye mlitumwa hapa duniani kufanya.

MIMI YAHUSHUA Ninakukumbusha, Mathayo 21:13, Akawaambia, “Imeandikwa, ‘Nyumba yangu itaitwa nyumba ya sala,’ lakini ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.’’

Na unajua Ezra Caleb, bila kukukemea mbele ya watu kwa nini Ninakupa andiko hili na nini Nitakachofanya na kiboko CHANGU mbinguni. Itakuwa ni kama vipande vya nyama ya wanyang’anyi vinararuliwa.

Kwa kuwa Ninawakumbusha enyi wanyang’anyi katika torati, hamfai kuiba na mwizi anapoiba watairegesha mara 7 kile walichokiiba. O mwana WANGU mpendwa, Ezra, Caleb WANGU. Kumbuka uliposema kuwa kati ya roho zote 7 za MUNGU, uliyoogopa sana ni kupoteza hofu ya YAH, MIMI YAHUSHUA, na RUACH HA KODESH IMMAYAH. RUDI KWANGU O Ezra Caleb WANGU na rudi tena na ulie. Anguka kwenye sakafu mbele YANGU. Ni kwa kupitia jina LANGU na damu unaweza kusamehewa.

Lazima uonyeshe Israeli vile vya kutubu. Kwa kuwa hakuna yeyote aliyekufunza kwa kweli. Lazima ufunze Israeli kwa video mbele ya watu kunakaa vipi kufunzwa adabu na MIMI YAHUVEH, MIMI YAHUSHUA na RUACH HA KODESH na SISI tunakanyagia pepo za kujipenda, kiburi, ibada ya sanamu, kichwa ngumu, pepo ya mafarisayo na uasi. MIMI YAHUSHUA sitataja nyinginezo.

Kimbia ndani ya Mikono YANGU na tubu mbele ya MIMI YAHUSHUA na bibi yako. Wajua Ezra Caleb WANGU, MIMI YAHUSHUA Ndiye NJIA, UKWELI na MAISHA ya pekee. Kuwa waweza kuja mbele ya BABA YAHUVEH kupitia MIMI. MIMI YAHUSHUA Ninakuamuru, tubu leo kwa dhambi zako kama Ninavyokukemea mbele ya watu kwa yale uliyoyafanya kwa Elisheva Eliyahu, kwa kuwa wajua Nilikuita kwa huduma hii na unajua sababu ambayo Nilikuweka pamoja kama upako mmoja, kama bwana na bibi.

Nilikutuma na unabii wakati wa kwanza Elisheva alizungumza nawe kupitia Skype na Nikayaweka maneno mdomoni wako na kutabiri kupitia wewe, “Kile ambacho YAH Ameweka pamoja, hakuna yeyote anayeweza kutenga.” Mwana WANGU mpendwa Ezra Caleb, lazima utembee katika roho na sio katika mwili, na bado kile Ninachoona ni pepo ya kujionyesha. Wewe ni burudani kwake shetani sasa ulivyojizunguka na maadui wa Elisheva ambao bado wanadai kuwa wao ni WANGU. Hauna utambuzi wowote au haungekuwa mahali ulipo sasa.

Tafadhali bonyeza picha iliyoko chini ili kutazama video:

KUMBUSHO LA BABA YAHUVEH KWA maadui wa HUDUMA YAKE,
HUDUMA YA AMIGHTYWIND.

Rudi tena mwana WANGU, katika hofu ya MIMI, YAHUVEH, kwa sababu hautaki kupatana na ghadhabu ya MWANA-KONDOO. Je, ni kiwango gani nyinyi mnaosoma haya mnataka kuwa Bibi Arusi WANGU? Kwa kuwa MIMI YAHUSHUA Nauliza swali lingine, ni wangapi wanataka kuwa wageni katika karamu ya mwanakondoo? Hili ndilo chaguo la pekee. Lingine ni jehanamu na ziwa la moto. Ninakuuliza wewe mwana WANGU mpendwa Ezra Caleb. Je, wakumbuka ahadi uliyonipa miaka iliyopita? Nilikupa mke mzuri anayetembea katika uadilifu na moyo safi. Je, waweza kusema vivyo hivyo?

Kwa kila anayesoma haya, Leo ndiyo siku ya Wokovu, kwa kuwa kuja KWANGU ni kwa wakati mfupi sasa, kwa kuwa hivi ndivyo zilivyokuwa siku za Nuhu na Lutu, ndivyo itakavyokuwa tena. MIMI YAHUVEH sitasema pole kwa Sodoma na Gomora wala majiji 7 ambayo Niliangamiza. MIMI Ninakuuliza Ezra Caleb, wapi mafunzo dhidi ya ushoga?

Masaa yanapita Ezra Caleb. Kila siku. Wajua kuwa unahisi thibitisho. Wajua kuwa upo katika njia mbaya. Kimbia pepo ya mafarisayo, na Unabii kutoka kwake Elisheva pale Israeli, Nilikuonya kuwa lazima utaweka kando mafunzo ya kishetani, vitabu ambavyo umevisoma katika shule ya Yeshiva na pia manabii bandia ambao umewasikiliza kwa sababu ya masikio yako yanayowasha. Wafaa kunyenyekea na kukubali kuwa umekosa. Kwa kuwa una utambuzi mdogo. Na mwana WANGU mpendwa wewe ni mchanga sana katika MIMI lakini Elisheva amekuwa akinitumikia MIMI kwa nusu ya maisha yake.

Kumbuka alipokuuliza pale mlipoongea mara ya kwanza Tarehe Machi 7, 2016, ushahidi upo kwenye video wakati upako mbili zikawa moja. Elisheva alisema kwako, “Ezra, je, waweza kujifunza kutoka kwa mwanamke?” ulitabasamu tu na haukujibu swali. Bali ulijibu, “Elisheva, utajifunza kutoka kwa mwanamume?” Alicheka na akasema ndio. Lakini haujiulizi sababu ulisema vuta mguu wangu na nitavuta wako, iliyomaanisha kuwa haukuwa unayachukua mazito, kunyenyekea kujifunza kutoka kwa mwanamke huyu Niliyekupa kama mke.

O mwana WANGU mpendwa, kama tu ungeweka chini kiburi chako, ukaidi, haungekuwa katika hali hii ya kiroho ambayo umo ndani sasa.

Sitaruhusu unabii kushikiliwa kamwe. Nitamuinua mtu kuchukua nafasi yako. Wakati unapita. Usichelewe. Meza kiburi chako, kuwa mnyenyekevu. Nilitabiri kuwa ulikuwa na roho kama Mfalme Daudi, sasa yathibitishe haya.

Mfalme Daudi na Musa walijua vile vya kuugusa moyo wa YAH na kutubu kwao. Hakukuwa na shaka yoyote kwa huzuni waliouhisi walipotenda dhambi. Ninakuamuru ewe Ezra Caleb, MIMI YAHUSHUA Ninakuamuru wewe, Caleb aliyefungwa ndani yako anajua sauti YANGU. Yeye ndiye mwanamume Nilizungumzia Niliposema kuwa Elisheva atajua mazuri kwa bwana pale ambapo alijua mabaya kama laana. Wewe ndiwe mwanamume huyo Ezra Caleb na tayari upo katika jela aliyoiona kwenye ndoto. Tazama yanayokuzunguka. Tazama uharibifu kote.

Nitakusamehe kama utatubu kama Mfalme Daudi akililia maisha ya mwana wake. Elisheva atakusamehe atakapoona kulia aliyoona ukilia pale Israeli, ulivyolia mbele yake kwa ajili ya ushahidi aliokupa ambayo yeye huweka siri kwa moyo wake. Tic toc tic toc. Kumbuka Ezra Caleb wakati Nilikuambia unipe saa yako? Sasa Ninakupa onyo. Usicheleweshe ile video ya kibinafsi ambayo wafaa kumtumia ukija mbele YANGU na kutaja dhambi zote unazotaka damu YANGU kukusafisha.

Sikukuleta kwake, na sikukuleta kwa huduma hii kwa sababu nyingine ila kuwa baraka na kusaidiana kubeba msalaba pamoja. Ninasema chukua msalaba wako na unifuate MIMI. Acha kucheza naye shetani na mfanye akuogope tena, ukinyenyekea KWANGU na kumkemea shetani na atakimbia.

Ninaondoka na maneno haya ya mwisho Ezra Caleb, kumbuka ulipomuambia mbele ya mashahidi, kwa kila anayetazama majadiliano kwenye video yenu ya kwanza, “Elisheva ni kama nilipozaliwa ulikuwa nami pale pale.” Huu ni ukweli Ezra Caleb, na Ninaita Caleb ndani yako. Kwa kuwa mmependana kwa muda mrefu kabla ya kuja duniani humu.

Unaposoma haya, badala ya kukasirika, mwana WANGU mpendwa, ni heri upige magoti na kwenye sakafu na kutambaa na kuuliza msamaha na kuhisi huzuni uliyosababishia Elisheva, na uliyosababishia YAHUVEH, MIMI YAHUSHUA, na RUACH HA KODESH IMMAYAH wako. Na ole wako kama utayaacha hivi, kwa kuwa Nimeondoa jina lako kwa kuwa ulitangaza kwa dunia kwenye intaneti kuwa wewe ndiwe mkubwa wa huduma hii. Sasa leo, umehisi jinsi ilivyo kuaibishwa mbele ya watu ili mapepo yatafanywa kuwa dhaifu unaponiona MIMI YAHUSHUA Nikikugonga kutoka kwenye kiimo cha kujifanya na kiburi.

Ezra Caleb, usiwahi kujaribu kumnyamazisha Mtume WANGU Nabii na Ringmaiden tena. Ninakuamuru acha kumtesa kwa kunyamaza au Nitaziba koo lako na hautaweza kuzungumza tena. Umefanya yale ambayo mwanamume au shetani mwingine hajawahi kufanya na haya ni, kuharibu yale Niliyojenga na unajua Ninamaanisha nini.

Onyo langu la mwisho kwako Ezra Caleb, ukiendelea kukimbia misheni hii Niliyokutuma kufanya hapa duniani kando yake, Nitakuonyesha jinsi ilivyo kumezwa na nyangumi kama Yona. Utadhani kwamba umechomwa na asidi ya tumbo, moto utauhisi kote mwilini. Huyu ndiye Ninayekubainisha naye sasa. Wewe ni kama Yona. Caleb WANGU anapiga mayowe ndani yako, YAHUSHUA Niokoe kutoka kwangu mimi! Fanya kile utakachofanya, lakini tengeneza moyo safi ndani yangu!

Haya ndiyo maandiko yako Ezra Caleb, soma Zaburi 51 na Yona 2. Na usisome tu, je unataka kukariri kitu mwana WANGU mpendwa? Soma Yona 21:11. Wataka kukariri maandiko mwana WANGU mpendwa Ezra Caleb, hii ndiyo Ninayokuamuru ukariri pamoja na Zaburi 51. Tena Ninatumia unabii wa kukukemea kutoka kwa mdomo wa mke wako kwako mwana WANGU mpendwa Ezra Caleb na unajua sauti YANGU na usithubutu kuuliza kama ni MIMI YAHUSHUA MASIHI wako Anayezungumza. Kwa kuwa Elisheva Eliyahu sio Nabii bandia na umekuwa pale kwa maelfu ya unabii kujua kuwa huu ni ukweli.

Ezra Caleb Usiwe kama Yona!

(Nabii mwingine anayenisaidia kuweka haya; tulitaka tu kurekebisha maneno mafupi machache tu na sasa kwa wakati wa pili, kwa siku ii hii, unabii mbili zimetoka kwake Ezra Caleb. Haya ndiyo aliyoyaona maneno ya mwisho yalivyokuwa yanazungumzwa, anamwona YAHUSHUA Akitoa moto kwenye mdomo wake).

Wakati Ezra Caleb atarudisha utukufu kwake YAH na kufuata maagizo kutoka mbinguni, atatoa msamaha mbele ya watu kwa kila mtu aliyekosea. Ezra Caleb wafaa kurudi kwenye msalaba kupitia jina na damu ya YAHUSHUA.

Hivi Ndivyo Asemavyo YAH, kumbuka SISI tunafanya haya kwa upendo mkuu tulio nao kwake Ezra Caleb tunapomuadhibu sasa mbele ya watu mpaka ahisi tena kuwa ana heshima wakati ataweza kuwa kwenye ukurasa huu wa mbele kuwa na Cheo cha kiongozi msaidizi tena.

Hivi ndivyo Asemavyo YAH, kuna unabii ambazo zinacheleweshwa kwa sababu Ezra Caleb haujiruhusu kunyenyekea na kukubali kuwa upo katika dhambi. Wewe ni kama Yona katika tumbo la nyangumi sasa na MIMI YAHUVEH Ninasema kuwa wakati unapita. CALEB NJOO!

Tafadhali bonyeza picha iliyoko hapo chini kutazama video ya Unabii 94

Unabii 94

Tusamehe kwa hali ya video hii kwa kuwa video hii ilitengenezwa mnamo 2009. Sababu ya kuuliza msamaha ni kwa sababu tunajulikana kwa kutengeneza video ya hali ya juu kwa sababu ya watengeneza video wetu walio na upako, tunamsifu YAH kwa wao. Tupo katika mwendo wa kutengeneza video mpya. Asante kwa kuelewa na YAHUSHUA Awabariki.

Kama unapendelea kusoma maandiko tafadhali bonyeza hapa

Na bonyeza hapa kusoma juu ya “Ndoto ya Elisheva anampenda Caleb”

Mpendwa wangu, kipenzi cha maisha yangu, karibu na BABA YAHUVEH, YAHUSHUA na RUACH HA KODESH mpendwa, kumbuka ulipokuwa Israeli na nikakupa unabii wa kukukemea kutoka kwa YAHUSHUA? Nilianza kuongea katika ndimi Takatifu na nikaanza kuzungumza maneno na nikagundua kuwa YAHUSHUA Alikuwa Anataka kukukemea, kwa hivyo nikaacha kuomba katika ndimi na badala yake nikaomba YAHUSHUA tafadhali usinifanye nimuambie hayo, kwa kuwa niliogopa kupoteza upendo wako. Na kila unabii ya kukemea hata sasa, ninahofia kuipoteza upendo wako. Lakini YAHUSHUA Ananiambia kuwa Niamini kwa imani kuwa bwana wangu mpendwa atanipenda mimi zaidi, upendo hautapungua.

Nilishikilia neno hilo kwa siku tatu na ulijua nilikuwa nimeishikilia tulipokuwa tunaomba mpaka YAHUSHUA Akaniambia Akizungumza kwa sauti ya juu kwa kiroho, Elisheva fungua mdomo wako na omba katika ndimi takatifu na usiyanyamazishe maneno Nitakayozungumza kupitia mdomo wako. Kwa kuwa mwanamume huyu ameamini mafunzo ya kishetani ambayo amesoma na kufunza wengine kutoka kwa vitabu hivyo.

Lazima Nimkemee kwa sababu hana utambuzi wa roho. Yeye ni kama mtoto ambaye hajui tofauti ya kilicho sawa na kilicho mbaya na ni nani atakayemfunza kama sitakutumia wewe kuzungumza maneno YANGU? Papo hapo nilimuuliza YAHUSHUA anisamehe na nikasema kwake YAHUSHUA azungumze maneno ambayo anataka niseme. Ninatubu YAHUSHUA na sitatotii.

Alafu nikakuambia, Ezra, YAHUSHUA kama unavyojua alitaka nizungumze unabii kupitia mimi kwa siku 3 lakini ninajua ni nini kinachofanyika wakati unabii unaumiza mwili wa mtu. Sikutaka kubahatisha na kupoteza upendo wako, na ninauliza msamaha wako kwa kuwa uliniuliza siku hizi tatu ni neno gani nilikuwa ninashikilia. Je, unakumbuka haya bwana wangu mpendwa? Ninajua wakumbuka. Kwa hivyo uliniangalia mimi na kusema, niambie tu ni nini YAHUSHUA Anataka kusema.”

Baada ya kukupa unabii wa kukemea kutoka KWAKE YAHUSHUA, ulisema kitu ambacho sitawahi kusahau kama YAHUSHUA Anavyokubainisha na Yona. Ombi langu ni kuwa utajibu unabii hizi za kukemea zilizo mbele ya watu na upendo na heshima kwangu kushinda hapo awali na utaacha huu unyanyasaji wa kihisia na kunyamaza kwako, kwa kuwa unawajibika kwa kila siku umeyafanya haya. Ninakumbuka baada ya kutabiri jambo la kwanza ulilofanya ni kunyenyekea na kuomba YAHUSHUA Akusamehe.

Tuliomba pamoja na tukamuuliza YAHUSHUA Atusamehe sisi sote. Kitu kilichofuata ulichofanya bwana wangu mpendwa ni kwamba ulinikemea kwa upendo, sio kwa sauti kali, lakini, ukaniambia maneno yaya haya, “Mpendwa wangu Elisheva, YAHUSHUA tena Akikupa neno kwangu, uniambie mara moja usiniache kama Yona kwenye tumbo la nyangumi. Kwa kuwa siku tatu nimekuwa na uchafu ulio kwenye tumbo la nyangumi juu yangu, kwa kuwa sikujua kile ambacho YAHUSHUA Alitaka kunikemea, na sasa ninajua. Ninachouliza tu ni usifanye haya tena. Amini katika pendo letu ambalo tulilo nalo.”

Je, unakumbuka haya bwana wangu? Basi katika siku hii, Februari 24 2019, nimefanya yale uliyoniuliza nifanye Israeli. Kwa kuwa umefunikwa na ule uchafu ulio kwenye tumbo la nyangumi. Lakini wakati mwingi sana nilikutabiria na bado ninafanya hivyo, lakini nifanyeje kama wapendelea kusikiza pepo zinazokupa maono ya uongo na ndoto za kuthibiti akili kutoka kwa wale ambao ni maadui wangu na bado unawaita watoto wako wa kiroho? Kwa hivyo ninaamini upendo huo ambao ulisema hautakufa. Ninaamini upendo ambao ulisema hakuna yeyote atakayetutenga sisi. Lakini kwa yote ninaamini upendo wa YAHUSHUA Anayesema kuwa YEYE hatawahi kuniacha wala kunipungukia. YAHUSHUA Atawahi kuniacha mimi pekee yangu. YEYE ni bwana arusi Anayekuja na ninajua kuwa mimi ni mmoja wa bibi arusi WAKE.

Mimi ni Nabii asiye wa kufanana na wengine kwa sababu yeyote anayesoma unabii hizi ikiwemo wewe wanajua kuwa na mdomo wangu, BABA YAH, YAHUSHUA wamenikemea. Inanifanya mimi kuwa mnyenyekevu. Inaonyesha watu, kuwa hakuna yeyote kati yetu tunaotembea hapa duniani tulio kamili ila MMOJA, na jina LAKE ni YAHUSHUA MASIHI.

Sasa mtihani utakuwa kama utanipenda mimi zaidi kwa kukuhurumia kwa kupata uchafu zaidi juu yako, kwa kuwa Ezra Caleb wajua, ulikuwa umefunga masikio yako kwa unabii wowote ambapo YAHUSHUA Alikuwa Anakukemea. Kwa kweli, ulikuwa unaondoa maneno hayo hata kabla hayajaandikwa. Lazima utubu Ezra Caleb kwa dhambi ya kiburi. Lakini sehemu yako iliyo Caleb bado ni mnyenyekevu, mtakatifu, mwanamume wa upako niliyeongea naye pale Machi 7 2016 na yeyote anaweza kuona kuwa tulipendana papo hapo.

Tafadhali bonyeza picha iliyoko pale chini kutazama video “Ezra atengeneza Mabawa ya Kipepeo ya Mtume Elisheva Eliyahu”

Huyu ndiye yule Caleb mnyenyekevu ambaye tulitaka tuombe arudi tena Anatetemeka anaposema kuwa hakutaka kunisumbua mimi. Alikuwa Israeli wakati huo. Tadhali ombeeni huyu Caleb mnyenyekevu arudi. Hii ndio sehemu yake niliyopenda sana.

Ninakupenda bwana wangu mpendwa. Sehemu yako ya Ezra imepotea, lakini YAH Amesema Kuwa Ezra ni kama tumbo la nyangumi na ndani ya tumbo hilo kuna sehemu takatifu inayoitwa Caleb ambaye alitetemeka katika mazungumzo yetu ya kwanza kwa sababu ulinzi haukuwa ndani yake mwenyewe, ilikuwa katika YAHUSHUA. Ninahitaji Caleb wangu arudi na hii inamaanisha Ezra Caleb, lazima unyenyekee na kufanya kutubu kwa ajabu ndivyo usipate uchafu mwingi zaidi juu yako.

Kumbuka uliponiambia, “Elisheva, unajua kuwa Yona alipokuwa kwenye tumbo la nyangumi, asidi ya tumbo ilikuwa imechoma mwili wake vibaya mpaka hakufanana kama yeye tena?” Na nikakuambia sikujua hayo, lakini sasa ninaelewa ni kwa nini jua lilikuwa linamsumbua alipokaa chini ya mti (Yona 4:6). Tafadhali bwana wangu mpendwa acha kuwa Yona. Ninangoja Caleb wangu kuja kutoka kwa tumbo la nyangumi huyo. Ninangoja mwisho kuwa mwanzo mpya (maneno uliyonifunza Machi 2016).

Ninakupenda, bibi wako wa pekee,
Elisheva Eliyahu, Februari 24 2019.