UNABII 136
UTATU TAKATIFU WANAHITAJI KUFARIJIWA PIA!
Ilizungumzwa katika Upako wa RUACH HA KODESH Kupitia Mtume Elisheva Eliyahu
Mei 29, 2017]
Neno hili lilitolewa siku kabla ya Shavu’ot 2017, jina la Kiebrania la Pentekoste.
* * * * * * *
Chini ni Unabii jinsi ilivyonenwa
– na “Ndimi Takatifu” za Nabii Ezra na Elisheva, kama vile ROHO wa MUNGU Anatoa matamshi (Matendo ya Mitume 2: 3-4) ya ndimi za Mbinguni au za Kidunia (1 Wakorinto 13: 1). Elisheva huongea kwa ndimi akileta Unabii (1 Wakorinto 14: 6). Ezra huanza maombi na ndimi za maombi (Warumi 8:26-27; 1 Wakorinto 14:15)
Tunatumia Majina ya Kiebrania ya MUNGU:
YAH/YAHU ni JINA TAKATIFU la MUNGU yaani “Alleluia” au “Hallelu YAH,” ambayo humaanisha “Sifu YAH”: YAHUVEH/YAHWEH MUNGU BABA; YAHUSHUA/YAHSHUA MWANA WA PEKEE WA MUNGU – (HA MASHIACH inamaanisha “MASIHI”; ELOHIM inamaanisha “MUNGU.”
Ufunuo wa “SH’KHINYAH GLORY” – kama JINA BINAFSI ya RUACH HA KODESH, Kwa Kiiengereza Anaitwa “HOLY SPIRIT” – pia ipo kwenye tovuti hii. (HA SH’KHINAH {SHEKINAH} ni Kiebrania kumaanisha UWEPO wa MUNGU UNAODUMU na wa UUNGU.)
Kuongezea, ABBA YAH inamaanisha “BABA YAH” na IMMA YAH inamaanisha “MAMA YAH.” Katika Kiebrania, ROHO WA MUNGU Ana jinsia ya kike, Anatajwa kama “SHE,” na amefananishwa vivi hivi kwenye Unabii na Maandiko yaliyo chini.
Maandiko yaliyotajwa ni ya KJV au NKJV isipokuwa pale palipotajwa vinginevyo.
* * * * * * *
Maneno ya YAHUVEH kwake Elisheva yafaa kuongezwa kabla ya Unabii:
Nilikuonya kitambo Elisabeth [Elisheva],
Kutoita Huduma hii kwa jina la mwanamume au mwanamke.
Hata kabla kuwepo na Huduma, niliiweka ndani ya roho yako.
Kwa kuwa hakuna lolote kwa haya lililofanyika kwa mkono wako.
Hakuna lolote lililotoka kwenye kinywa chako.
Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUVEH Aliyeizalisha.
Ilitoka kwenye Kinywa cha YAHUSHUA, MASIHI wako Aliyeizalisha.
Ilitoka kwenye Kinywa cha RUACH HA KODESH, IMMAYAH wako Aliyeizalisha.
Kama ingekuwa tu kwa mkono wako, ingekuwa imefeli kitambo.
Ni kwa UPEPO WA SHKHINYAH GLORY Unaovuma kote duniani, UPEPO TAKATIFU WA UAMSHO.
Sio kwa pumzi yako, au ingekuwa imefeli.
“MIMI Ndiye BWANA YAHUVEH: hilo ndilo JINA LANGU:
Na UTUKUFU WANGU sitampa mwingine,
Au SIFA ZANGU kwa Sanamu za kuchonga.” Isaya 42:8
(UNABII WA 105)
Katika mwezi wa Julai 2010, YAHUVEH MUNGU pia Alisema kuongezwe yafuatayo kama onyo kwa wale wanaokejeli:
Lakini waliwadhihaki Wajumbe wa MUNGU, na kuyadharau Maneno YAKE, na kuwacheka Manabii Wake, hata ilipozidi Ghadhabu ya Bwana juu ya watu WAKE, hata kusiwe na kuponya.
—2 Mambo ya Nyakati 36:16
Alafu, Julai 2016:
Ole kwa yeyote atakayethubutu kujaribu kuwadhuru— hawa wawili walio na upako. Mtajuta kuzaliwa kwenu. Msiwaguse masihi WANGU, msiwadhuru Manabii WANGU (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22). Ingekuwa ni heri kwenu kama MIMI, BABA YAHUVEH, Ningerarua ndimi zenu!
(Unabii wa 128)
Na kutoka Nabii Ezra:
Nawaonya nyote—nyote mnaokuja dhidi ya Huduma hii NA UNABII HIZI na Elisheva na mimi, Wahudumu wa Huduma ya Amightywind—Nawaonya nyote sasa, Msiwaguse Masihi wa YAH, msiwadhuru Manabii WAKE’ (Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) kabla Ghadhabu za Gongo la YAH zije juu yenu. Lakini kwa wale waliobarikiwa na wao ni baraka katika Huduma hii, na ni waaminifu, na wamepokea Unabii hizi, baraka tele zitakuja juu yenu—yote kulinda yale ambayo ni ya YAH katika JINA la YAHUSHUA.
* * * * * * *
UNABII 136
UTATU TAKATIFU WANAHITAJI KUFARIJIWA PIA!
Unabii huu ulirekodiwa kupitia sauti. Huu ndio usajili.
[Ezra aomba katika Ndimi Takatifu…]Elisheva: Zinapendeza. O BABA YAHUVEH tunakushukuru na tunakusifu katika JINA la YAHUSHUA MASIHI tunavyokuja mbele ya kiti CHAKO cha Enzi na shukrani na sifa! Asante kwa shavu’ot [sikukuu ya majumaa]! Asante kwa kuhesabu kwa omer! Asante kwa wakati huu wa mavuno. Asante BABA YAHUVEH kuwa [kama] Unavyoleta shavu’ot, WEWE pia wakati huu husherehekea BABA wa MBINGUNI kuwa Uliniletea mimi kiongozi mpya wa kiume BABA wa MBINGUNI katika JINA LA YAHUSHUA. Hivi ndivyo Unavyobariki sio Huduma YAKO tu lakini pia wabariki Nabii WAKO.
Haya ni zaidi, zaidi ya upendo BABA wa MBINGUNI kwa sababu YAHUSHUA, WEWE haukuenda tu kwenye Msalaba na kumwaga DAMU YAKO kwa UPATANISHO wa dhambi zetu. Kwa kuwa hakuna yeyote kati yetu, hakuna yeyote kati yetu duniani humu aliye kamili. Lakini badala ya haya, BABA wa MBINGUNI na MPENDWA YAHUSHUA, Pia Ulisema, YAHUSHUA, kuwa hautatuacha sisi yatima (Yohana 14:18)
na Ulipoondoka, WEWE Ulisema pia Utamtuma MSAIDIZI. (Yohana 15:26; 16:7) MSAIDIZI Atakuja.
Na Ukawaambia wanafunzi WAKO kungoja na kuhesabu siku hadi chumba cha juu na Uliwapa tarehe ya kuwa pale na Ukasema kuwa MSAIDIZI Atakuwepo.
Yohana 14:17-18
Huyo ndiye ROHO WA KWELI ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa sababu haumwoni wala haumjui. Ninyi mnamjua kwa kuwa yuko pamoja nanyi naye anakaa ndani yenu. Sitawaacha ninyi yatima, naja kwenu.
Yohana 15:26
Lakini atakapokuja huyo MSAIDIZI nitakayemtuma kwenu kutoka kwa BABA, yaani, huyo ROHO WA KWELI atokaye kwa BABA, Yeye atanishuhudia MIMI.
Tunajua MSAIDIZI ni NANI. Ni ROHO MTAKATIFU. Ni MPENDWA, MPENDWA ROHO MTAKATIFU, RUACH HA KODESH kwa Kiebrania, na IMMAYAH. Tunakushukuru na tunakusifu IMMAYAH! Tunakusifu BABA YAHUVEH! Tunakusifu YAHUSHUA kwa kuyafanya haya!
O, Ninaulizia Neno sasa. Ni nini, Neno hili, Unalotaka kusema leo Shavu’ot? Kwa siku 7 tutasherehekea BABA wa MBINGUNI kuwa [leo Shavu’ot 2016] Ulileta huyu kiongozi mpya wa kiume, na Nabii Mwisraeli — ambaye sasa ni mume wangu mpendwa ambaye tuliolewa Oktoba 2, 2016 na ilikuwa siku ya Rosh ha Shana, wakati tulikuwa tunakungojea WEWE YAHUSHUA kurudi siku ya Rosh ha Shana. Kwa kuwa WEWE Ndiwe BWANA ARUSI wetu wa kwanza.
Na tunakungojea WEWE na tunakuuliza ni nini wataka kusema sasa? Tafadhali, ni nini kilicho Moyoni MWAKO? Kwa kuwa tunataka watu waje na wapate kukujua WEWE zaidi. Wanahitaji kukujua zaidi. Hawajifunzi WEWE NI NANI BABA YAHUVEH, ambao WENGINE huita “Jehovah” lakini JINA LAKO ni YAHUVEH. NYINYI mna MAJINA ya KIEBRANIA na Huduma hii hufunza MAJINA haya ya KIEBRANIA.
Ni nini wataka kusema? Ni vipi tunavyoweza kufanya watu kukujua WEWE zaidi — kujua kuwa WEWE sio tu MUNGU wa GHADHABU lakini WEWE ni MUNGU WA UPENDO na UVUMILIVU na FADHILI ZA MILELE.
Lakini huwa kunakuja wakati wao huvuka mpaka wanapoirusha DAMU, DAMU ya UPATANISHO ambayo YAHUSHUA Alimwaga pale Kalivari kwenye Uso YAKE na kusema, “Ninataka kuifanya kwa njia yangu! Nitaishi maisha haya kwa njia yangu! Na sitafanya chochote Kitakatifu kwa kuwa hamna raha.”
Lakini WEWE una Neno la kusema na Ninataka kujua, tunahitaji kujua — kama bwana yangu alivyoomba katika Ndimi Takatifu na zilikuwa Ndimi Takatifu za ulinzi (Warumi 8:26-27; 1 Wakorinto 14:15) panaposema ‘Msiwaguse Masihi WANGU na msiwadhuru Manabii WANGU’
(Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22) —ni nini Unachotaka kusema BABA YAH? Kwa kuwa Manabii hawajabwagwa! Bado sisi tupo na sisi ndio Macho YAKO na sisi ndio Masikio YAKO na tunataka kujua.
Warumi 8:26-27
Vivyo hivyo, ROHO hutusaidia katika udhaifu wetu, kwa sababu hatujui kuomba ipasavyo, lakini ROHO MWENYEWE hutuombea kwa uchungu kusikoweza kutamkwa. 27Naye Mungu aichunguzaye mioyo, anaijua Nia ya ROHO, kwa sababu Roho huwaombea watakatifu sawasawa na mapenzi ya MUNGU.
1 Wakorinto 14:15
15Nifanyeje basi? Nitaomba kwa roho, lakini nitaomba kwa akili yangu pia. Nitaimba kwa roho na nitaimba kwa akili yangu pia.
Zaburi 105:15 na Mambo ya Nyakati 16:22
15Akisema, “Msiwaguse masihi wangu,
msiwadhuru manabii wangu.’’
[ Elisheva anaomba katika Ndimi Takatifu… ]
Unabii 136
UTATU TAKATIFU WANAHITAJI KUFARIJIWA PIA!
Shavu’ot 2017
Unabii Unaanza:
Huyu ni BABA YAHUVEH wenu! Ninapenda mnaponiita MIMI “BABA”. MIMI NI BABA YENU MPENDWA! Nilimtoa MWANA WANGU WA KIPEKEE ili mrudi Mbinguni tena. Kwa kuwa hakuna yeyote, hakuna yeyote aliye kamili! YAHUSHUA pekee Ndiye kamili, AMBAYE wengine humwita “YESU KRISTO”. Lakini Ninataka mmwite YEYE “YAHUSHUA”, kwa JINA LAKE la KIEBRANIA.
Mtapata ya kwamba kuna Nguvu na Upako zaidi katika JINA la KIEBRANIA, lakini bado kuna nguvu na upako katika Jina la ‘YESU KRISTO’.
Tafadhali, Ninataka kuwajua zaidi katika siku hii ya Shavu’ot wanayoiita Siku ya Pentekoste. Wengi wanataka kusema tu, “Ni Siku ya Pentekoste tu” —na huu [Unabii] utatolewa siku ya Shavu’ot —hilo ndilo sababu Ninaiita Shavu’ot. Hili ndilo ombi LANGU kwenu nyinyi watoto WANGU. Haya ndiyo Ninayowauliza watoto WANGU.
Watoto WANGU! Watoto WANGU! Watoto WANGU! Watoto WANGU! Watoto WANGU! Watoto WANGU! Ninataka kuwajua zaidi! MIMI NI MUUMBA WENU! Hakuna mwingine! Msiwahi kuweka dini pamoja!
Haya sio mambo ya dini! Haya yanahusu uhusiano na MUUMBA wako. Haya yanahusu MASIHI wako, MWOKOZI wako YAHUSHUA Aliyelipa GHARAMA pale Kalivari — ili kutoka jehanamu [uokolewe], usiende, ili Niweze kusikia maombi yenu tena, ili Niweze kusamehe dhambi zako —YEYE Alimwaga DAMU YAKE! Kwa kuwa DAMU YAKE ilikuwa kamili! Ilitoka Mbinguni!
YEYE sio tu MWANA WA MUNGU MWENYEZI, MIMI YAHUVEH! YEYE sio tu MWANA WA IMMAYAH (RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU MPENDWA)! YEYE ni MUNGU pia! Sote WATATU ni MOJA! (1 Yohana 5:7; Yohana 1:1-2; 10:30; Mithali 8:23, 27, 30) Wafunze mtoto WANGU! Wafunze!
1 Yohana 5:7
Kwa maana wako WATATU washuhudiao Mbinguni: Hao ni BABA, NENO na ROHO MTAKATIFU, nao hawa WATATU ni WAMOJA.
Yohana 1:1-2 na 10:30
1Hapo mwanzo, alikuwako NENO. Huyo NENO alikuwa pamoja na MUNGU, naye NENO alikuwa MUNGU. 2Tangu mwanzo huyo Neno alikuwa pamoja na MUNGU.
30MIMI na BABA YANGU tu UMOJA.
Mithali 8: 23, 27, 30
23Niliteuliwa [HEKIMA, ROHO MTAKATIFU] tangu Milele, tangu Mwanzoni, kabla ya dunia kuumbwa. […]27Nilikuwapo alipoziweka mbingu mahali pake, wakati alipochora mstari wa upeo wa macho juu ya uso wa kilindi, […] 30Wakati huo nilikuwa fundi stadi kando yake
nilijazwa na furaha siku baada ya siku,
nikifurahia daima mbele ZAKE.
Waambie waangalie yai! Ni sehemu gani ndiyo yai? Nilikufunza haya kutoka mwanzo! Nitakuambia uifunze tena. Waambie. Waambie mtoto WANGU. Angalia yai! Je, yai ni ganda?
Je, yai ni kiini cha yai? Je, yai ni sehemu nyeupe?
Ni sehemu gani ndio yai? Ni yote! Yai ni yai.
SISI WATATU, UTATU ni MOJA! (1 Yohana 5:7) MIMI BWANA, MUNGU WENU ni MOJA! BABA YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH (RUACH HA KODESH, ROHO MTAKATIFU), SISI ni MOJA! Haya ndiyo Ninayotaka kuwafunza siku ya Shavu’ot!
Kumbukumbu laTorati 6:4
Sikia, Ee Israeli: BWANA YAHUVEH ni MUNGU wako, BWANA YAHUVEH ni MMOJA.
AU
Sikia, Ee Israeli: YAH ni MUNGU wako, YAH ni MMOJA.
Haya ndiyo Ninayotaka Wayahudi kuelewa! Hawawezi kugombana wanapotazama yai. Ninazungumza kana kwamba wao ni watoto sasa. Ninazungumza kana kwamba nyote ni watoto, kwa sababu nyinyi ni watoto! (Matendo ya Mitume 17:28) Nyinyi ambao hudhani mnajua mengi, mnajua madogo sana (Ayubu 38:2; 1 Wakorinto 3:19-20).
Matendo ya Mitume 17:28
‘Kwa kuwa katika YEYE tunaishi, tunatembea na kuwa na uzima wetu’. Kama baadhi ya mashairi yenu yalivyosema, ‘Sisi ni watoto WAKE’
Ayubu 38:1-2
Kisha BWANA YAHUVEH akamjibu Ayubu kutoka katika upepo wa kisulisuli. Akasema: “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa?
1 Wakorinto 3:19-20
19Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za MUNGU. Kama ilivyoandikwa: “MUNGU huwanasa wenye hekima katika hila yao,” 20Tena, “BWANA YAHUVEHanajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni ubatili.”
Ninataka kuwafunza kama mtoto — Huduma hii inapaswa kufunzwa kana kwamba kila mtu ni mtoto. (Mathayo 11:25; Luka 10:21) Njooni KWANGU sasa — kama mtoto. (Marko 10:15) Tuanze tena.
Luka 10:21, ona Mathayo 11:25
21Saa ile ile, YAHUSHUA akashangilia katika ROHO Mtakatifu akasema, “Nakushukuru BABA, BWANA WA MBINGU NA NCHI, kwa sababu mambo haya umewaficha wenye hekima na wenye akili, nawe umewafunulia watoto wadogo. Naam, BABA, kwa kuwa hayo ndiyo yaliyokuwa mapenzi YAKO.
Marko 10:15
Amin, amin nawaambia, mtu yeyote asiyeukubali Ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo, hatauingia kamwe.”
Msiamini yale ambayo yanafunzwa sasa kuwa dini zote zinaweza kuja pamoja. (1 Wakorinto 8:5-6; 2 Wakorinto 6:14; Yohana 14:6) Hapana! Hapana! Hapana! na Hapana!
1 Wakorinto 8:5-6
5Kwa maana hata kama wapo hao wanaoitwa ‘miungu’ kama ni Mbinguni au duniani, (kama ilivyo kweli wapo ‘miungu’ wengi na ‘mabwana’ wengi). 6Lakini kwetu sisi yuko MUNGU MMOJA, aliye BABA, AMBAYE vitu vyote vyatoka KWAKE na kwa ajili YAKE sisi twaishi na kuna BWANA MMOJA tu, YAHUSHUA MASIHI, AMBAYE kwa YEYE vitu vyote vimekuwepo na kwa YEYE sisi tunaishi.
2 Wakorinto 6: 14
Msifungiwe nira pamoja na watu wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa, kwa maana pana uhusiano gani kati ya haki na uovu? Au kuna ushirika gani kati ya nuru na giza?
Yohana 14:6
6YAHUSHUA akawaambia, “MIMI NDIMI NJIA na KWELI na UZIMA. Mtu hawezi kuja kwa BABA isipokuwa kwa kupitia KWANGU.
Wale ambao wanamwita “Allah” au “Mohammed” — UPATANISHO wa dhambi upo wapi? Kwa kuwa hakuna kusamehewa kwa dhambi bila Damu ya Upatanisho (Mambo ya Walawi 17:11; Waebrania 9:22).
Mambo ya Walawi 17:11
11Kwa kuwa uhai wa kiumbe uko ndani ya damu nami nimewapa hiyo damu ili mfanyie upatanisho kwa ajili yenu wenyewe juu ya madhabahu, damu ndiyo ifanyayo upatanisho kwa ajili ya maisha ya mtu.
Waebrania 9:22
22Kwa kweli sheria hudai kwamba, karibu kila kitu kitakaswe kwa damu, wala pasipo kumwaga damu, hakuna msamaha [wa dhambi].
YAHUSHUA Ndiye wa PEKEE Aliyelipa GHARAMA! Na YEYE Alichukua hiyo nafasi ya mwanakondoo wa pasaka! YEYE Ndiye MWANAKONDOO WA PASAKA! YEYE Aliuliwa wakati sawa na yule mwanakondoo wa pasaka aliyeuliwa! (Hesabu 9:2-3)
Hesabu 9:2-3 (JPS)
Waamuru Waisraeli waadhimishe Pasaka katika wakati ulioamuriwa. Adhimisheni wakati ulioamuriwa, yaani wakati wa kuzama jua siku ya kumi na nne ya mwezi huu, kufuatana na desturi zake zote na masharti yake.
Na YEYE Aliwekwa kwenye msalaba na Aliteswa na Alichapwa na Aliaibishwa na Akabeba aibu yako na kila udhaifu, kila ugonjwa! (ona Isaya 53)
Alifanya haya kwa ajili yenu watoto WANGU lakini hakufa tu — kwa kuwa hakuna yeyote aliyeweza kuchukua maisha YAKE (Yohana 10:18-19) kama Alivyokuwa pale msalabani kwa masaa 3, kama asiyekuwa na hatia! Msafi na Mtakatifu! Hata fikra ya dhambi haikuweza kuingia Kichwani MWAKE (ona Waebrania 4:15 nk)!
Yohana 10:17-18
17BABA YANGU ananipenda kwa kuwa ninautoa uhai WANGU ili niupate tena. 18Hakuna mtu aniondoleaye uhai WANGU, bali ninautoa kwa hiari yangu mwenyewe. Ninao uwezo wa kuutoa uhai WANGU na pia ninao uwezo wa kuutwaa tena. Amri hii nimepewa na BABA YANGU.’’
Ingawa Alijaribiwa na shetani kwa siku arobaini,
(ona Mathayo 4: 1-2; Marko 1:13; Luka 4:1-2) hata mara moja, hakuna fikra ya dhambi iliyoingia Kichwani MWAKE. Muwe Watakatifu! Ishi kwa Utakatifu! Alitoa Maisha YAKE kwa ajili yenu lakini haimaanishi kuwa mwanadamu alichukua Maisha YAKE. (ona Yohana 10:18-19 pale juu). Hata YEYE Ndiye Aliyesema, “Imekwisha”! na Akafa. Yohana 19:30)
Yohana 19:30
[…]YAHUSHUAkasema, “Imekwisha.’’ Akainamisha kichwa CHAKE, akakata ROHO.
Lakini Ninataka msherehekee siku ya Shavuot! Katika siku ya 3 Alithibitisha kuwa YUKO hai! (1 Wakorinto 15) Na Aliingia kwenye mlango uliokuwa umefungwa (Yohana 20:19) ambapo wanafunzi wake walikuwa wamejificha na kuhuzunika. Kwa kuwa Alijionyesha
baada ya kuenda jehanamu na kuwajulisha shetani na pepo kuwa wameshindwa! (Waefeso 4:8-10) Walikuwa wameshindwa kwa kuwa YEYE ni MUNGU MWENYEZI!
YEYE ni BWANA na MWOKOZI wenu! YEYE ni MWANA WANGU! Lakini YEYE huvaa Cheo cha “BWANA MUNGU MWENYEZI”! YEYE ni MASIHI! YEYE ni MWOKOZI! Na wanafunzi walifurahia kama Ninavyowauliza mfurahie siku ya Shavu’ot. Kwa kuwa mwaona YEYE hakuwaacha bila kusema kuwa Atamtuma MFARIJI. YEYE Alijitokeza mbele ya wanafunzi na kusema, ‘Ninamtuma MFARIJI!’ (Yohana 16:7). Na MFARIJI Ndiye ROHO MTAKATIFU MPENDWA.
Sasa Ninawaambia siri siku hii ya Shavu’ot.
Wengi wenu hamjui — na nyinyi ambao hamjui chochote cha Bibilia — maneno haya Ninayoyazungumza sasa: Lazima kwanza mtubu. Pigeni magoti mbele YANGU. Hapo awali sikuweza kusikia maombi yenu kwa kuwa ilifaa YAHUSHUA Asulubiwe na kutoa DAMU YAKE MWENYEWE kuchukua nafasi yako kwa ule msalaba pale Kalivari. YEYE Aliteseka kwa ajili yako! Kwa hivyo unapokiri na kutubu dhambi zako na kwa kweli unajaribu vile iwezekanavyo kuishi katika Utakatifu mbele YANGU, ukitii sio tu Amri 10 pekee, lakini pia Amri za Torati, ambazo ni maagizo kamili ya YAHUSHUA zinazotumika wakati wa sasa.
Kutubu inamaanisha kusema pole. Sio kama [Rais] Donald Trump alivyosema kabla hajajua bora hakuwahi kuuliza asamehewe. Sasa anajua kuwa lazima aulize msamaha. Wote lazima waulize msamaha.
O siku ya Shavu’ot ni wakati Mtakatifu sana! Na kuhesabu kwa omer — kama hamjakuwa mkiyafanya haya — hata YAHUSHUA Aliyafanya haya. O inamaanisha wakati wa kuvuna!
Kuna mengi zaidi Ninayotaka kuwafunza lakini sio sasa. Nitazungumza Unabii zaidi kuhusu haya. Sasa hivi Ninataka mjue jinsi, jinsi, jinsi SISI tunavyohitaji faraja yenu pia.
Sasa Ninazungumza na wale ambao wameokoka, kusafishwa na kujazwa na ROHO MTAKATIFU, RUACH HA KODESH MPENDWA. Ninazungumza kwa wale wanaofanya juu chini ili wasinikosee MIMI. Hawa ndio Ninaotaka kuzungumza nao. SISI Tunahitaji faraja yenu. Je, mnajua ya kwamba UTATU TAKATIFU Tunahitaji faraja yenu?
Ninazungumza kwa Watoto, Bibi Arusi, Waliochaguliwa na Wateule. Nyinyi huja KWETU na mnahitaji faraja na SISI tupo papo hapo! Mnakuja kwetu na maombi yenu na SISI tupo papo hapo. Mnaniuliza MIMI na mnapokea, kwa sababu SISI tupo papo hapo.
Lakini, hamwelewi? Sisi hulia. MIMI, YAHUVEH hulia. YAHUSHUA hulia. IMMAYAH hulia. SISI hulia! SISI hucheka nanyi! SISI tunataka kucheka nanyi! SISI tunataka kucheza nanyi. Nyinyi ni watoto! Ni baba yupi hataki kucheza na mtoto wake? Ni baba yupi hataki mtoto wake kumuuliza maswali? Ni baba mzuri mgani? Ni baba Mtakatifu mgani?
MIMI sizungumzi kwa yeyote ila tu wale ambao kwa kweli ni wa YAHUSHUA MASIHI. Wale wengine hata hawataelewa. Na kwa wale wasioelewa, Neno hili sio lenu kwa hivyo hata msisikize. Hata msijaribu kupiga kelele. Hata msijaribu kumwita nabii bandia kwa kuwa Nishawaonya kwa uwazi, ‘Msiwaguse Masihi WANGU wala kuwadhuru Manabii WANGU’
(Zaburi 105:15; 1 Mambo ya Nyakati 16:22).
Ninataka uhusiano na wapendwa WANGU. MIMI sitaki MNIOGOPE tu — lakini kuogopa ndio mwanzo wa Hekima (ona Mithali 9:10; Zaburi 111:10) — Ninataka mnitii MIMI.
Mithali 9:10
Kumcha BWANA YAHUVEH ni mwanzo wa Hekima na kumjua [YULE] MTAKATIFU ni Ufahamu.
Zaburi 111:10
Kumcha BWANA YAHUVEH ndiyo chanzo cha Hekima, wote wanaozifuata amri zake wana busara. Sifa ZAKE zadumu milele.
Jitahidi, Jitahidi, Jitahidi kuishi maisha Matakatifu! Na unapofeli — na hivi karibuni tu mtakuwa kama watoto wasiotii na mtafeli lakini tubuni — ulizeni msamaha na msifikirie kuwa YAHUSHUA Alifariki pale msalabani ili kuwapa kisingizio ili mueze kutenda dhambi tena. Nyote mtawajibika kwa yote mnayoyajua. (Mathayo 12:36)
Mathayo 12:36
36Lakini nawaambia, katika Siku ya Hukumu watu watatoa hesabu kuhusu kila neno lisilo maana walilonena.
Daudi alikuwa mwanamume aliyetafuta Moyo WANGU kwa sababu moja. (ona 1 Samueli 13:14; Matendo ya Mitume 13:22) Alijua kutubu. Alihuzunika na kulia na aliuliza msamaha. Na Niliweza kuzungumza kupitia yeye na Niliweza kuzungumza naye. Na Ninataka kuzungumza nawe.
Sasa Nitawauliza Elisheva na Ezra, huyu Nabii Mwisraeli ambaye sasa ni bwana wa Elisheva na kiongozi wa kiume wa Huduma hii — Nilimchagua yeye, Nilimteua, Nilimpa upako kuchukua nafasi ya yule bandia aliyekuwa na hata akaacha kuniamini MIMI muda wa miaka 7 iliyopita. Wokovu wa nepi haina maana!
Wokovu wa baiskeli ya miguu mitatu haina maana! Hii ni baiskeli ya mtoto mdogo. Wao huanza kwa kujaribu kufanya yaliyo sawa — alafu wao huniacha MIMI. Wao huacha Utakatifu. Wao husema, “Ni ngumu sana kuifanya njia ya YAHUVEH.”
O lakini wewe Ezra na Elisheva, mnanifurahisha MIMI! Mnanifurahisha MIMI kwa sababu nyinyi hujaribu na nyinyi wote wengine Ninaowazungumzia sasa ambao ni watoto wa YAHUSHUA MASIHI — kwa sababu ya GHARAMA iliyolipwa pale Kalivari — kwa sababu mnaamini kuwa YEYE hakubaki kaburini lakini katika siku ya 3 Alifufuka; na YEYE Alipanda Mbinguni; na Alirudi tena na maagizo kwa wanafunzi wake; na kama Alivyopanda Atarudi tena (Matendo ya Mitume 1:11) na msijaribu kuweka tarehe pale.
Matendo ya Mitume 1:11
[Malaika] wakasema, “Enyi watu wa Galilaya, mbona mnasimama mkitazama juu Mbinguni? Huyu YAHUSHUA aliyechukuliwa kutoka kwenu kwenda Mbinguni, atarudi tena jinsi iyo hiyo mliyomwona akienda Zake Mbinguni.’’
Lakini Ninawaambia haya. Tazameni ishara zilizo duniani, tazameni ishara za angani. (ona Mathayo 24; Marko 13; Luka 21 nk) Someni kila Unabii na kuila. Kwa kuwa mwaona haya sio maneno tu. Binti YANGU ambaye anatabiri sasa, ambaye ni Mtume, Nabii na Ninayemwita Ringmaiden WANGU, alianza hapa mtandaoni mwaka wa 1995 ambapo MIMI YAHUVEH Nilizaa Huduma hii kuleta nafsi kwake YAHUSHUA MASIHI, sio moja kwa moja lakini kwa mamilioni wakati mmoja — katika lugha tofauti hata hawezi kufuatilia nambari tena.
Na hata kama kitabu kimeandikwa kinachoelezea ROHO MTAKATIFU NI NANI na — Siri za ROHO MTAKATIFU iliyochukua muda mrefu kuandika, kuiunganisha na Maandiko —je, mwafikiria HEKIMA ni nani? (oneni Vitabu vya Hekima) Je, ni kwa nini katika Bibilia ya Mfalme James (King James Version Bible) inamwita SHE? (oneni Mithali 1-9) Je, Hawa aliumbwa katika mfano wa nani (Mwanzo 1)? Niliposema tumuumbe mwanadamu katika Mfano “WETU”, MIMI sikusema Mfano “WANGU”. Nilisema Mfano “WETU (Mwanzo 1:26). Sio MIMI tu, bali pia IMMAYAH. Na huyu IMMAYAH Ndiye mfano wa Hawa. Na nyinyi wanaume mliumbwa katika mfano wa MIMI YAHUVEH, na YAHUSHUA.
Kwa hivyo, wafunze! Wafunze hata katika siku ya Shavu’ot. Niimbieni MIMI. Imbieni UTATU TAKATIFU! Msiingie tu katika maombi na kuuliza maswali lakini imbeni, sifu! Ingieni katika Nyua ZANGU Mbinguni mbele ya Kiti CHANGU cha Enzi na heshima, upendo na ibada katika JINA LA YAHUSHUA (Zaburi 100:4)! Usiwahi kufikiria waweza kuingia katika UWEPO WANGU katika jina lenu wenyewe (Waebrania 4:14-16). Kwa kuwa Nitasikiza tu katika JINA LA YAHUSHUA, AMBAYE wengine humwita ‘YESU KRISTO’. (Matendo ya Mitume 4:12) Lakini Ninawasihi, jifunzeni JINA la KIEBRANIA sasa kabla halijatumiwa vibaya katika Dhiki Kuu.
Zaburi 100:4
Ingieni malangoni MWAKE kwa shukrani
na katika nyua ZAKE kwa kusifu,
mshukuruni YEYE na kulisifu jina LAKE.
Matendo ya Mitume 4:12
Wala hakuna wokovu katika mwingine awaye yote, kwa maana hakuna JINA jingine chini ya Mbingu walilopewa wanadamu litupasalo sisi kuokolewa kwalo.’’
Ezra na Elisheva mnanifurahisha sana MIMI kwa kuwa hamniimbii MIMI tu, hamwombi tu KWANGU lakini Elisheva mnafanya mengi zaidi. Nyote wawili, mnafunza yote ambayo Nimewapa. Mnaongoza nafsi kwa MWANA WANGU YAHUSHUA. Na YAHUSHUA, WEWE huleta nafsi hizo KWANGU. Nilisema sitapoteza hata mmoja.
Wakati majina yanaandikwa katika Kitabu cha Maisha cha Mwanakondoo, pia kuna Kitabu cha Waliolaaniwa na pia Kitabu cha Waliofutwa
(Ufunuo wa Yohana 20:11-12; pia ona Zaburi 69:28 nk).
Ufunuo wa Yohana 20:12
Nami nikawaona wafu wakubwa na wadogo, wakiwa wamesimama mbele ya hicho kiti cha enzi na vitabu vikafunguliwa. Pia kitabu kingine kikafunguliwa ambacho ni cha uzima. Hao wafu wakahukumiwa sawasawa na matendo yao kama yaliyoandikwa ndani ya hivyo vitabu.
Lakini Ninazungumzia Kitabu cha Maisha na wakati jina linaandikwa na umekufa moyo na umerudi nyuma — tayari Nishayaona haya kama Warumi 8 inavyosema kwa uwazi (Warumi 8:29; 9:22 nk) jina tu linapoandikwa, linafutwa papo hapo ni kama halikuwahi kuwa hapo na linajitokeza kwenye Kitabu cha Waliolaaniwa.
Warumi 8:29
Maana wale Mungu aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa MWANAWE, ili YEYE awe MZALIWA WA KWANZA miongoni mwa ndugu wengi.
Warumi 9:22-23
22Iweje basi, kama MUNGU kwa kutaka kuonyesha ghadhabu YAKE na kufanya uweza WAKE ujulikane, amevumilia kwa uvumilivu mwingi vile vyombo vya ghadhabu vilivyoandaliwa kwa uharibifu? 23Iweje basi, kama YEYE alitenda hivi ili kufanya wingi wa UTUKUFU WAKE ujulikane kwa vile vyombo vya rehema YAKE, alivyotangulia kuvitengeneza kwa ajili ya UTUKUFU WAKE.
Hizi ndizo siri Ninazowaambia siku hii ambazo ni kuu zaidi ya maombi Niliyosema hapo awali, Niliyokuwa Nimekuambia uombee. Omba jina lako lisiwahi kupatikana katika kitabu cha Waliofutwa kwa kuwa ni heri uwe tayari umewekwa kwenye Kitabu cha Waliolaaniwa. Kwa kuwa hili ndilo zawadi la pekee utakalopokea — katika dunia hii, ni kuishi maisha yako, ukimtumikia shetani, ukifanya vitu kwa njia yako kwa miaka mifupi tu halafu ni jehanamu na ziwa la moto.
O lakini nyinyi ambao hufuata njia YANGU! Nyinyi mpo katika Kitabu cha Maisha milele! Na mnasema, “Sitaifanya kwa njia yangu kwa kuwa sio mimi ninaoishi lakini ni WEWE YAHUSHUA Unayeishi maisha YAKO ndani yangu” (linganisha na Wagalatia 2:20) na WEWE huifanya njia ya YAHUVEH.
Wagalatia 2:20
Nimesulibiwa pamoja na YAHUSHUA wala si mimi tena ninayeishi bali YAHUSHUA ndiye aishiye ndani yangu. Uhai nilio nao sasa katika mwili, ninaishi kwa imani ya MWANA WA MUNGU, aliyenipenda na kujitoa kwa ajili yangu.
Kwa hivyo Ninataka mchukue wakati kutufariji SISI. Je, mnajua kuwa MUNGU WA VIUMBE VYOTE, MUNGU WA WOKOVU na IMMAYAH, ROHO MTAKATIFU — bila ROHO MTAKATIFU hamngeweza kuja kwake YAHUSHUA
(Yohana 16:8-9; 1 Wakorinto 12:3; Yohana 3:5; ona pia Ufunuo wa Yohana 22:17; Waebrania 10:29; 1 Yohana 5:6-7; Mithali 1:20-23; 8:1-4; Mithali 9:10; 19:8; 8:35-36)? YEYE NDIYE Anayekuongoza. YEYE NDIYE Anayekuvuta, au hata haungejali.
Yohana 16:8
8Naye atakapokuja, atauthibitishia ulimwengu kuhusu dhambi, haki na hukumu.
1 Wakorinto 12:3
3[…] Pia hakuna mtu awezaye kusema, “YAHUSHUA ni BWANA,” isipokuwa ameongozwa na ROHO MTAKATIFU.
Yohana 3:5
5YAHUSHUA akamwambia, ‘‘Amin, amin nakuambia, hakuna mtu ye yote anayeweza kuingia katika Ufalme wa MUNGU isipokuwa amezaliwa kwa maji na kwa ROHO.
Sasa Ninataka mjue yale ambayo manabii wengine hawajasema. Je, mnafikiria SISI tunahisi vipi wakati hata Jina la ‘YESU KRISTO’ linatumika kama matusi? Wakati MIMI na YAHUSHUA na hata wote — IMMAYAH ROHO MTAKATIFU MPENDWA na Bibilia, Maandiko Matakatifu yote yanakejeliwa? Ni wangapi wachache ambao wanaotaka kuishi katika Utakatifu?
Sasa Kitabu CHETU — Kitabu mnachokiita Bibilia — lakini kwa kweli kinaitwa Maandiko Matakatifu kwa kuwa sio kitabu kimoja tu. Kuna vitabu vingine kama kitabu cha Enoki. Wanaziita “Vitabu vya Bibilia Vilivyopotea” lakini si vyote vilivyopotea. Vinaweza kupatikana kama tu mtavitafuta.
Maktaba ya Vitabu Vya Bibilia Vilivyopotea
Ninataka kuwafunza. Ninataka kuwafunza kuwa lazima muwe na ushuhuda kama wa Enoki.
(Waebrania 11:5-6) Kwa kuwa hakuona kifo lakini alitembea NAMI. Na alikuwa rafiki YANGU na hakuona kifo. Badala ya hayo, alinyakuliwa na kuenda Mbinguni (Mwanzo 5:23-24).
Waebrania 11:5-6
5Kwa imani Enoki alitwaliwa [hadi Mbinguni] kutoka katika maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, kwa sababu MUNGU alikuwa amemchukua. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza MUNGU. 6Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU, kwa maana ye yote anayemjia MUNGU lazima aamini kwamba YEYE yuko na ya kuwa HUWAPA THAWABU wale wamtafutao kwa bidii.
Mwanzo 5:23-24
23Enoki aliishi jumla ya miaka 365. 24Enoki akatembea na MUNGU, kisha akatoweka, kwa sababu MUNGU alimchukua.
Alitembea NAMI. Malaika, kama Enoki alivyokuwa kwenye mgongo wao, walimbeba hadi Mbinguni — mahali alipowaona [kati ya] malaika wabaya [waliofungwa], ili Ningeweza kuwaonya sasa. (ona Siri za Enoki 18:1-4) Kuna Mbinguni na kuna jehanamu na kuna mahala ambapo malaika wabaya wapo.
Na maadui wa Huduma hii, Ninawaambia haya, [Saa Sita za usiku Mei 27-28 2017] vita vimekadiriwa kutoka Mbinguni
msipotubu!
Na kwa waliokataliwa, [waliolaaniwa] — na mnajijua nyinyi ni nani — nyinyi hamwachukii hawa Manabii tu, uongozi lakini Ninawaambia haya: wao hufuata amri kutoka kwangu YAHUVEH tu kwa kweli UTATU tu NDIYE UONGOZI lakini ilibidi Niwe na mtu hapa duniani kama Nilivyofanya katika vitabu vya kale, kuwa mdomo WANGU. Na huyo ndiye huyu Nabii. Yeye husikia kutoka KWANGU. Manabii WANGU wa Kweli watazungumza Utakatifu.
Manabii WANGU wa Kweli hawataogopa kukera — kwa minajili ya nafsi yako — jifunzeni haya!
Siku ya Shavu’ot [au Pentekoste], walipoanza kuomba katika ndimi (Matendo ya Mitume 2:4) —wanafunzi waliokusanyika Ghorofani (ona Matendo ya Mitume 1-2) — na mashahidi walioshuhudia haya, walipokusanyika na kukejeli na hata wakasema kuwa walikuwa wamelewa (Matendo ya Mitume 2:19), lakini ni karama kutoka Mbinguni ili mueze kunisikia MIMI vizuri (1 Wakorinto 14:6)! Lakini sio — kuwa kama hauna karama ya ndimi, inamaanisha kuwa haujaokoka. (1 Wakorinto 12:4-12; 13:1) Msiamini uongo huu.
Matendo ya Mitume 2:1-4
1Ilipowadia Siku ya Pentekoste, walikuwa wote mahali pamoja. 2Ghafula sauti kama MVUMO MKUBWA WA UPEPO uliotoka mbinguni, ukaijaza nyumba yote walimokuwa wameketi. 3Zikatokea ndimi kama za moto zilizogawanyika na kukaa juu ya kila mmoja wao. 4Wote wakajazwa na ROHO MTAKATIFU, wakaanza kunena kwa lugha nyingine, kama ROHO alivyowajalia.
Mmeokolewa mnapojitahidi kutii kila Neno YAHUSHUA Asema na MIMI YAHUVEH na mnapopiga magoti na mnasema, “Njoo moyoni mwangu. Njoo maishani mwangu. Njoo nafsini mwangu. Njoo mwilini mwangu. Njoo akilini mwangu. YAHUSHUA tawala. Ishi maisha YAKO kupitia mimi. Kwa kuwa ulitoa maisha YAKO ili niweze kupata uhuru kutoka kwa shetani na pepo na kutoka jehanamu! WEWE Uliyafanya haya kwa njia ambayo hakuna yeyote anayeweza kukana.”
Ndiyo kwa sababu hata herufi B.C. (Before CHRIST/KABLA KRISTO) haijafutwa kutoka wakati wa historia kwa kuwa wanajua kuwa YEYE Aliishi. Na bado YEYE Anaishi na yuko hai.
MIMI, YAHUVEH, Nazungumza nanyi sasa. SISI tunahitaji kufarijiwa! Tuimbie SISI! Mtatuimbia SISI tafadhali? Mtatulilia SISI tafadhali?
Je, mnajua kuwa wanayaita Maandiko Matakatifu sasa kuwa ‘hadithi’ tu’? Je, mnajua ni wangapi katika dunia hii waliogeuka hata kwa kuamini katika hiki Kitabu Kitakatifu kinachoitwa Bibilia, Tanakh. Wanacheka Amri ZANGU za Torati, zile zinazotumika leo— kwa kuwa kumbukeni wale ambao ni Watoto WANGU wanaelewa ni yapi yanayotumika sasa. Lakini Amri 10 (Kutoka 20:1-17; Kumbukumbu la Torati 5:4-21) hamwezi kutoroka. Kwa kuwa mwafaa kumpenda BWANA MUNGU wenu — juu ya yote — na hii inamaanisha UTATU TAKATIFU.
Usizungumze tu kwa BABA, MIMI YAHUVEH, lakini zungumza kwake YAHUSHUA YEYE Aliyelipa GHARAMA pale Kalivari na zungumza kwake IMMAYAH ROHO MTAKATIFU MPENDWA Anayewangoja, kuwa Nitangaze mbele ya dunia YEYE ni nani. YEYE ni HEKIMA (Mithali 1-9; ona pia Vitabu vya Hekima).
Mithali 3:15-18
15Hekima ana thamani kuliko marijani,
hakuna cho chote unachokitamani
kinachoweza kulinganishwa NAYE.
16Maisha marefu yako katika Mkono WAKE wa
Kuume,
katika Mkono WAKE wa Kushoto kuna utajiri
na heshima.
17Njia ZAKE zinapendeza,
mapito YAKE yote ni amani.
18YEYE ni MTI WA UZIMA kwa wale
wanaomkumbatia, wale wamshikao watabarikiwa.
Sasa Ninawaambia siri nyingine ambayo Niliambia Elisheva kitambo. Kila siku aliamka— na kumbukeni Huduma hii imekuwa kwenye mtandao kupita miaka 22 lakini alianza kabla ya wakati huu — kuniuliza MIMI, “Ni nini wataka nijue leo?”
Na Nikampa maagizo haya ambayo Ninawapa nyinyi sasa, kama mtachagua kuyafanya. Kutakuwa na baraka ndani yake na tena sizungumzi na wapagani, Ninazungumza na wale wanaonijua MIMI kwa kweli na MWANA WANGU na wanaojua ROHO MTAKATIFU ni nani. Kwa wale wengine, hamtaelewa.
Chukueni Bibilia hiyo, iliyo na binder laini inayoweza kufunguka, na ombeni juu ya Bibilia hiyo. Ombeeni ulinzi. Kemea shetani na mhakikishe kuwa hamna dhambi yoyote ndani, kuwa mmeuliza msamaha kwa dhambi yoyote. Na mnafanya haya baada ya ushirika. Haya ni maagizo mapya Ninayowapa leo hii ya Shavuot mwaka wa 2017. Kwa kuwa Ninapenda kuwafunza mapya, hata kama kwa Elisheva ni ya kale.
Na mnasema, “BABA YAHUVEH Naja mbele YAKO kwa sifa, upendo na shukrani. Asante kwa MWANA WAKO YAHUSHUA kwa kuwa BWANA, MUNGU na MWOKOZI wangu. Kwa kuwa Neno linasema, ‘Mtiini BWANA YAHUSHUA na mpingeni shetani naye atawakimbia!’ (ona Yakobo 4:7). Kwa hivyo, Nalitaja Neno hili KWAKO. Kwa kuwa Neno LAKO haliwezi kukurudia tupu. (Isaya 55:11) Na ninakuuliza WEWE, tumia neno hili sasa. Zungumza nami. Fungua Bibilia hii sasa ninavyoomba Damu ya YAHUSHUA juu yake.”
Mnaweza hata mkapaka mafuta, juu ya Kitabu, na niulizeni MIMI, “Katika JINA LA YAHUSHUA, ROHO MTAKATIFU MPENDWA, RUACH HA KODESH, IMMAYAH, wataka nisome wapi leo? Ni nini Unachotaka kuniambia leo hii?” na ona unapoishika mikononi mwako kama imefungwa, ona kama sitaifungua.
Ona kama sitaifanya Mikono ya RUACH HA KODESH kuifungua. Lazima iwe na binder laini. Lakini tazama na ona vile itakavyofunguka polepole na Neno litakaloonekana kwa macho yako na mahala ambapo macho yako itaangukia, ndipo Ninapotaka usome.
Pengine itakuwa sura mzima uliyosoma tayari. Pengine itakuwa ni sentensi tu. Pengine unachotafuta ni neno moja tu. Ninataka kuzungumza nawe. Ninataka msome Neno LANGU Ninataka muone kuwa iko hai. Ninataka isikike!
“Ni nini Unachotaka kuniambia leo hii BABA YAH? Katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI, Ninaomba.”
Tazama na ona Nitakachofanya. Kama wakati huu sasa, MIMI huwaambia Elisheva na Ezra kitu ambacho bado hawajaelewa lakini Ninawapa maelezo. Kama sio wakati uo huo, endeleeni kuifikiria mpaka mpate ujumbe ambao Ninataka mjue. Na Nimewapa wao [sura ya] kwanza ya Ezekieli, mstari wa 17. Na hata Nimewaambia wageuze ukurasa. Ninataka wajue Neno fulani. Na Ninayasema haya sasa tu ili wakumbushwe. Lakini hata nyinyi mnaweza kuangalia.
Ezekieli 1:17
Yalipokwenda yalielekea upande wo wote wa pande nne walipoelekea wale viumbe, magurudumu hayakuzunguka wakati viumbe vile vilipokwenda.
Ninataka tu muanze siku yenu — bila visingizio —ya kusikia Maneno YANGU, hata kama ni kwa simu ya mkononi. Someni Maneno YANGU. Niulize MIMI, “Ni kitabu kipi wataka Nisome leo?” Hata kama ni katika [Agano la] Kale au [Agano] Jipya ambalo ni moja tu [Agano], niulizeni MIMI. Kwa kuwa itakuwa ni kitu ambacho Ninataka mjue ambayo mnahitaji kujua katika sehemu ya maisha yenu ambayo mliyomo.
Kwa wapagani, haya hayatawasaidia. Haya sio kama utabiri wa psychic. Ninazungumza haya Maneno kwa Watakatifu sasa. Ninataka kuwapa mengi zaidi kama mtayachukua. Na Ninataka kuwaonyesha kuwa Neno LANGU liko hai.
Na kuhusu Unabii, someni Unabii moja kila siku! Niulize MIMI Unabii upi. Na Ninawaahidi kuwabariki na kuwaonyesha.
Maneno YANGU yako hai! Andiko huua bali ROHO hutia uzima (2 Wakorinto 3:6)! ROHO MTAKATIFU huwapa maisha na haijalishi ni mara ngapi mtasoma Unabii mtaona tu kama Bibilia hiyo, Maneno yako hai.
2 Wakorinto 3:6
[MUNGU] YEYE ndiye aliyetufanya sisi kuwa wahudumu wa Agano Jipya, si wa andiko bali wa Roho, kwa kuwa andiko huua bali Roho hutia uzima.
Na mtayasoma Maneno na mtaona sentensi ambayo hamkuwa mmeielewa au kuifahamu hapo awali. Itakuwa ni kama yanajitokeza kwenye kurasa na yatakuwa maneno ambayo mnahitaji kujua katika sehemu hiyo ya maisha yenu.
Haya ndiyo Ninayotaka kuwafunza siku hii ya Shavu’ot, kwenye sherehe — sherehe! — ambapo maelfu waliokolewa (Matendo ya Mitume 2:41, 47 nk) ROHO MTAKATIFU MPENDWA Alipoanguka juu ya wengi wakati huo na wakazungumza katika ndimi mpya.
Haikuwa tu ndimi za binadamu, za lugha ya [wanadamu] ambayo hawakujua, ilikuwa pia ndimi za malaika. (1 Wakorinto 13:1) Na shetani hawezi kufahamu wala kuelewa, hata Maneno yanayozungumzwa sasa hivi. Kwa hivyo Nina hamu ya nyinyi kujifunza haya mafunzo sasa.
Maneno YANGU ni taa kwa miguu yenu. (Zaburi 119: 105) Niruhusu kuwaongoza kwa Maneno YANGU.
Zaburi 119:105
Neno lako ni taa ya miguu yangu na mwanga katika njia yangu.
Ni nyayo —hata katika giza totoro, masaa ya giza.
Waza maneno ya Zaburi 91: majibu yapo palepale hata kwa Wayahudi kama tu watafahamu; JINA LA YAHUSHUA lipo pale — likifunza Wokovu, likifunza Majina Takatifu, wale wanaolia katika JINA LANGU! Wayahudi, Nisikizeni MIMI!
Zaburi 91:14-16
14BWANA asema, “Kwa kuwa ananipenda nitamwokoa, nitamlinda kwa kuwa amelikubali JINA LANGU.’’ 15Ataniita, NAMI nitamjibu, nitakuwa pamoja naye katika taabu, nitamwokoa na kumheshimu. 16Kwa siku nyingi nitamshibisha na kumwonyesha WOKOVU WANGU.
Ni mtoto mgani ambaye hajui jina la baba yake? (Mithali 30:4)
Mithali 30:4
Ni NANI ameshapanda Mbinguni na kushuka? […] Ni NANI ameimarisha miisho yote ya dunia? JINA LAKE ni nani na MWANAYE anaitwa nani?
Niambie kama unajua!
— shetani amewadanganya! Hataki mtaje JINA LANGU.
Katika JINA LANGU na katika JINA LA YAHUSHUA, MWANA WANGU Aliyesulubiwa pale Kalivari na kufufuka kutoka wafu ili mpate kuwa huru, o wapendwa WANGU, Nisikilizeni MIMI!
Kitabu hiki sio hadithi tu! Na Ninaposema “Kitabu”, Ninazungumzia Maandiko Matakatifu, Bibilia, hata Vitabu Vilivyopotea (ona Maktaba) lakini vingine ni bandia kwa hivyo jihadharini — shetani kamwe huwa na bandia ya yale halisi.
Na mnapoomba pamoja na unapoomba pekee yako, uliza katika JINA LA YAHUSHUA, “BABA YAH, BABA YAH, ni yapi wataka kuniambia?”
Hata kama mtafanya haya wakati mmoja tu kwa siku. Lakini wakati mnapohitaji Neno kutoka KWANGU, mnapohitaji Neno la faraja, Niliwapa Kitabu hiki. Na wale wanaosema, “O kiliandikwa na binadamu,” ndio walewale watakaosema, “O Neno hili limetoka kwa mwanamke,” lakini, ni zaidi ya hayo (2 Timotheo 3:16; 2 Petro 1:21).
2 Timotheo 3:16-17
16Kila Andiko, LILILOVUVIWA NA MUNGU lafaa kwa mafundisho, kwa kuwaonya watu makosa yao, kuwaongoza na kuwafundisha katika haki 17ili mtu wa MUNGU awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila kazi njema.
2 Petro 1:20-21
20Awali ya yote, yawapasa mjue kwamba hakuna Unabii katika Maandiko uliofasiriwa kama apendavyo mtu mwenyewe. 21Kwa maana Unabii haukuja kamwe kwa mapenzi ya mwanadamu, bali watu walinena yaliyotoka kwa MUNGU wakiongozwa na ROHO MTAKATIFU.
Kumbukeni ni yale maneno ambapo macho yenu yatakapoangukia na pengine mtagueza ukurasa ili kuiweka muktadha ndani yake. Kumbukeni muktadha wa mistari mnayoyasoma, lazima itumike.
SISI ni UTATU TAKATIFU. Msiruhusu yeyote kuwaambia kuwa SISI sio. Na mnapoinama mbele YANGU YAHUVEH, mnainama mbele YAKE YAHUSHUA na IMMAYAH RUACH HA KODESH MPENDWA. Na SISI tutawainua na tutawaambia haya, nyinyi ni watoto katika MACHO yetu. Hamwezi kuja Mbinguni kwa njia nyingine ile — haijalishi elimu uliyo nayo. (Mathayo 2:3-4) Mtakapokuja Mbinguni, itawekwa kando na maneno tu Niliyoyazungumza yatasimama, Maneno ambayo YAHUSHUA Alizungumza. (Mathayo 24:35)
Mathayo 18:3-4
3Naye akasema: ‘‘Amin, nawaambia, msipoongoka na kuwa kama watoto wadogo, kamwe hamtaingia katika Ufalme wa Mbinguni. 4Kwa hiyo mtu yeyote ajinyenyekezaye kama huyu mtoto, ndiye aliye mkuu kuliko wote katika Ufalme wa Mbinguni.
1 Wakorinto 3:19-20
19Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuzi mbele za MUNGU. Kama ilivyoandikwa: “MUNGU huwanasa wenye hekima katika hila yao,” 20Tena, “YAHUVEH anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni ubatili.”
Sikilizeni IMMAYAH. Sikilizeni ROHO MTAKATIFU MPENDWA, Maneno ya HEKIMA AMBAYE Bibilia ya Mfalme James huita “SHE” (ona Mithali, Mathayo 11:19; Luka 7:35). Sikilizeni hayo maneno ili SISI tuweze kuzungumza. Na mnaposikia, msisikize tu, someni kwa sauti ya juu. Msisome tu kwenu nyinyi wenyewe. Mruhusu maneno hayo kutoka mdomoni mwenu. Na mjitahidi na kutii. Na mjifunze [kuwa] maagizo Niliyowapa lazima, lazima myatii.
Nyinyi ambao ni Bibi Arusi wa YAHUSHUA, tayari mnajua nyinyi ni nani kwa kuwa mnathamini Maneno haya. Mnathamini shavu’ot [wiki] — mnajua kuwa hamngeweza kuokolewa bila, sio tu, JINA na DAMU YA YAHUSHUA lakini [pia] ilibidi MFARIJI aje, ROHO MTAKATIFU MPENDWA. Sitawaacha! Niliwaambia haya!
SISI tunawathamini! Je, Mnajua kuwa sisi tunawathamini kila mmoja wa watoto WETU kitofauti?
Je, Mnajua haya? SISI tunawajua watoto wetu: SISI tunajua ni wapi mpo wanyonge; SISI tunajua ni wapi mna nguvu. IMMAYAH RUACH HA KODESH MPENDWA, ROHO MTAKATIFU, wakati mmeokoka kwa kweli, huishi ndani yenu — Atakosa kujuaje?
Na inalingana na yale ambayo uliyoyafanya. Je, Umefanyia YAHUSHUA nini? Ni nafsi ngapi ulizoleta kwake YAHUSHUA — hata kama mmemwambia mmoja tu?
Je, Mnajua kuwa YAHUSHUA huwapa NYINYI KAMA ZAWADI KWANGU?
Na [YEYE] husema, “BABA ona, Sitakosa hata mmoja ambaye jina lake limeandikwa katika Kitabu cha Uzima cha Mwana Kondoo. Haijalishi ni yapi lazima yafanyike, hata kama ni lazima niwashushe chini zaidi — hata kama wao wanafikiria kuwa maisha yao yameharibika — Nitawafanya waangalie juu na Nitawafanya watubu na kuuliza msamaha na kunikubali MIMI, DAMU YA UPATANISHO. Na Nitawaambia wao kutii na Nitawaambia Nimewasamehea.”
Alafu Nitawatoa kama zawadi KWAKO.
Alafu sasa chaguo ni lao kama wataendelea kutembea katika Utakatifu na kusikiliza Maneno Ninayozungumza na maneno haya yamo katika Maandiko Matakatifu. Chaguo ni lao na tayari imekadiriwa kama Warumi 8 inavyosema kwa uwazi.
Warumi 8:29
Maana wale MUNGU aliowajua tangu mwanzo, pia aliwachagua tangu mwanzo, wapate kufanana na mfano wa MWANAWE, ili YEYE awe MZALIWA WA KWANZA miongoni mwa ndugu wengi.
Na tena Ninasema, “Hapa Ninakuletea mwingine na Ninaleta mwingine.”
Lakini, Ninayafanya haya vipi? Ninatumia watoto WANGU. Ninawatumia kama Ninavyomtumia huyu anayezungumza sasa. Ninawatumia Manabii WANGU. Ninawatumia hata nyinyi ambao sio manabii.
Sio lazima uwe nabii kuleta nafsi Mbinguni. Zungumza ukweli tu ulio katika Maandiko Matakatifu. Waambie tu ni lazima watii Maandiko Matakatifu na mwaambie kuwa wanapoanguka, [wako na MASIHI] kwa kuwa hakuna yeyote ambaye ni kamili (Warumi 3:23) hata nabii huyu anayezungumza anahitaji MASIHI kwa kuwa hakuna yeyote aliye kamili. Lakini kutii Amri 10 ndiyo hatua ya kwanza lazima mchukue, alafu mtaenda kwenye Torati ambayo inatumika leo.
Mnaona kuwa YAHUSHUA ni MUNGU pia — kumbukeni kuwa SISI ni MOJA! Kumbukeni ni mara ngapi YEYE Alisema, Siwezi kufanya chochote ambacho sijaona BABA YANGU [akifanya], alichofanya na anachofanya. Siwezi kuzungumza chochote YEYE hazungumzi na asichozungumza (linganisha na Yohana 5:19-30)
Yohana 5:19
19YAHUSHUA akawaambia, Amin, amin nawaambia, MWANA hawezi kufanya jambo lo lote pekee YAKE, YEYE aweza tu kufanya lile analomwona BABA yake akifanya, kwa maana lo lote afanyalo BABA, MWANa pia hufanya hivyo hivyo. 20BABA ampenda MWANA na kumwonyesha yale ambayo YEYE BABA MWENYEWE anayafanya, naye atamwonyesha kazi kuu kuliko hizi ili mpate kushangaa. 30MIMI siwezi kufanya jambo lo lote PEKEE YANGU. Ninavyosikia ndivyo ninavyohukumu, nayo hukumu YANGU ni ya haki kwa kuwa sitafuti kufanya mapenzi YANGU mwenyewe, bali mapenzi YAKE YEYE aliyenituma.’’
Kwa kuwa YAHUSHUA hawezi kudanganya. MIMI YAHUVEH siwezi kudanganya na ROHO MTAKATIFU MPENDWA hawezi kudanganya. (Warumi 3:3-5) Kwa hivyo kumbukeni haya watoto wangu wapendwa.
Watoto, o watoto, o watoto, o watoto, mpo katika mwisho wa siku za mwisho — sasa —sio tu dakika chache zilizobaki, ni sekunde zilizobaki katika wakati WANGU. Na Ninawapa maagizo haya mapya.
Msikose kufanya ushirika. Ni kumbusho la GHARAMA, YAHUSHUA Alilipa pale Kalivari lakini kumbukeni kuwa lazima mtubu dhambi zenu kwanza. Lazima mtubu na lazima muishi maisha ya Utakatifu. Au watoto WANGU mtakuwa mnakunywa kikombe cha laana. (1 Wakorinto 11:28-29)
1 Wakorinto 11:28-29
28Inampasa mtu ajichunguze mwenyewe, kabla ya kula mkate na kukinywea kikombe. 29Kwa maana mtu ye yote alaye na kunywa pasipo kuutambua MWILI WA BWANA, anajiletea hukumu juu yake mwenyewe.
Kumbukeni haya watoto WANGU, ulizeni msamaha kabla hamjachukua mkate wa ushirika, kipande cha mkate, kile ulicho nacho kuwakilisha mkate ambao ni [mwili wa] mwili uliokuwa YAHUSHUA Aliyesulubiwa pale msalabani.
Na damu, ni upatanisho wa dhambi zenu. YEYE Alilipa GHARAMA. Tone moja tu ndio iliyotakikana tu kusafisha dhambi za dunia hii ambayo sasa zipo ndani kama tu watapokea haya.
Basi chukueni ile sharubati ya mzabibu au chukueni mlicho nacho. Nendeni mkasome maagizo ya ushirika, kila wakati ni tofauti — je, mtazungumza maneno ya upendo ya kurudia kwa mpendwa wenu, mchumba wenu? Zungumzeni na YAHUSHUA ni kama YEYE ni mchumba wenu kwa kuwa YEYE Ndiye MPENZI WA MAISHA YENU kama MIMI Nilivyo MPENZI WA MAISHA YENU, kama vile ROHO MTAKATIFU Alivyo MPENZI WA MAISHA YENU. Hakuna yeyote anayefaa kuja mbele.
Lazima mkumbuke daima, msipende karama Nilizowapa zaidi ya ALIYEWAPA MAISHA, MIMI MUUMBA na YAHUSHUA MASIHI wenu na RUACH HA KODESH MPENDWA. Watoto wenu, wachumba wenu lazima waje sehemu ya pili daima.
O watoto WANGU, watoto WANGU, watoto WANGU, Watoto WANGU! Watoto WANGU, Bibi Arusi WANGU, Wateule WANGU, nyote mnajaribiwa. Na mmejaribiwa kwa kiasi kubwa. Lakini kwa wale ambao mnafanya juu chini kuishi katika Utakatifu na kuacha mengineyo msalabani pale Kalivari na kumuuliza YAHUSHUA, “O niokoe na nisamehe,” mmesamehewa. Lakini jihadharini na makanisa yaliyopo sasa. (Yuda 1:4) Kwa kuwa wengi husema — ndio Nasema wengi watawaambia —— “Usijali kuhusu kutenda dhambi tena.”
Yuda 1:4
4Kwa kuwa kuna watu waliojipenyeza kwa siri katikati yenu, watu walioandikiwa tangu zamani hukumu hii, waovu, wapotoshao neema ya MUNGU wetu kuwa ufisadi wakimkana YEYE aliye BWANA WETU WA PEKEE, BWANA YAHUSHUA MASIHI.
Hamwezi kuweka dini zote pamoja. Je, Si YAHUSHUA Alisema kabla hajaondoka, kama neno linalosema, Maandiko Matakatifu, Bibilia, “Hamu YANGU ni nyinyi kuwa moja” (Yohana 17:20-23)? Huyu sio Mwislamu. Kwa kuwa hawampokei YAHUSHUA kama MASIHI. Wako na nabii wao, Mohammed na hayo hayatawaingiza Mbinguni.
Yohana 17:20-23
20“Siwaombei hawa pekee yao, bali nawaombea pia wale wote watakaoniamini kupitia neno lao 21ili wawe na umoja kama vile WEWE BABA ulivyo ndani YANGU na MIMI nilivyo ndani YAKO, wao nao wawe ndani YETU, ili ulimwengu upate kuamini ya kuwa WEWE ndiye uliyenituma MIMI. 22UTUKUFU ule ulionipa nimewapa wao, ili wawe na umoja kama SISI tulivyo wamoja. 23MIMI ndani YAKO na WEWE ndani YANGU, ili wawe wamekamilika katika umoja na ulimwengu upate kujua ya kuwa umenituma, nami nimewapenda wao kama unavyonipenda MIMI.
Kwa hivyo kile ambacho Trump amefanya — wakati ambapo hata Papa anajidai kuwa mungu [KIUNGO CHA Unabii 66] — Nitawaambia kwa siri wakati mwingine ni nini kinachoendelea.
Kwa kuwa yule Trump ambaye Elisheva alitabiri juu yake, kuna zaidi ya mmoja [Trump]. Clone wapo na doubles wapo. Kwa hivyo Nitawaelezea mengi kuhusu haya wakati mwingine.
Hamwezi kuchanganya Ukatoliki — yale ambayo papa huhubiri sasa na husema, anapobeba msalaba uliokunjwa unaokejeli YAHUSHUA na kujitangaza kama mungu na kuwa ana chochote cha kufanya na YAHUSHUA [Ombi la Wokovu] — na chochote kufanya na Maandiko Matakatifu. Kwa kuwa dhambi ni dhambi na haijabadilika hata katika nyakati hizi za kisasa ambayo mwafikiria mnaishi.
Kumbukeni kuwa majaribio ya imani yenu ni ya thamani sana kushinda dhahabu (1 Petro 1:7). Nyinyi mnaoteseka sana na mnashangaa ni kwa nini nyinyi ambao ni WANGU na mnaishi kwa Utakatifu mbele YANGU — na mnaabudu YAHUSHUA na JINA LAKE lipo midomoni mwenu daima na daima mnaomba na mnaleta nafsi KWANGU na mnanifanyia MIMI kazi — na bado mnateseka sana, kumbukeni haya. “Majaribio ya imani yenu [ni] ya thamani sana kushinda dhahabu” (1 Petro 1:7).
Kumbukeni Ayubu. Someni kitabu cha Ayubu. Kumbukeni “mengi ndio mateso ya watakatifu” (Zaburi 34:19) — Sikusema machache, Nilisema —mengi ni mateso ya watakatifu, lakini MIMI, BWANA MUNGU wenu YAHUVEH katika JINA LA YAHUSHUA MASIHI, Nitawaokoa kutoka kwa kila moja. Na kama sio hapa duniani, itakuwa Mbinguni.
Zaburi 34:19
Mwenye haki ana mateso mengi, lakini YAHUVEH humwokoa nayo yote.
Na Elisheva, Na sasa Ninazungumza nawe mpendwa WANGU Nabii wa Israeli Ezra, Mtume WANGU, kama nyote wawili mlivyo —na Ninazungumza na nyinyi wawili ambao ni Ringmaiden na Ringbearer, sasa vile bandia ameondoka, sasa Ninawaambia haya. Yeyote atakayejaribu kurarua huu uhusiano wenu wa bwana na bibi, Nitamwaga ghadhabu ZANGU chini tena zaidi. Na zitatoka Mbinguni.
Na Nitachukua maisha ya sio wao pekee katika njia ya kuumiza wakati ambao hawatakuwa wanatarajia, lakini Nitachukua chochote cha thamani ikiwemo kazi zao. (ona Kumbukumbu la Torati 28) Ninamaanisha chochote na yeyote ikiwemo watoto wao. [Haya pia] ni ya yeyote atakayejaribu kuharibu Huduma hii Takatifu ambayo si ya mwanamke au mwanamume yeyote, lakini kwa kweli ilizalishwa kutoka Mbinguni na yeyote atakayejaribu kupasua na kurarua Unabii hizi Takatifu ambazo haziji kutoka kwa mwanamke au mwanamume yeyote — Ninamtumia mwanamke huyu kama chombo Kitakatifu, Mjumbe Ninayeweza kumwamini, [pia] kama Ninavyomtumia mwanamume huyu Mtakatifu.
Haya ndiyo Nabii hufanya. Wananena siri ili msishangae ambapo wengine hawatafungua macho yao. Hamtapata kila kitu katika Kitabu Kitakatifu kinachoitwa Bibilia kwa kuwa kuna vitabu vingine kama Nilivyosema na moja yao ni Kitabu cha Enoki — na kuna vitabu vingine vilivyotajwa hata katika Maandiko ya Bibilia: Kitabu cha Yashari mliambiwa mjifunze na kusoma — ni wangapi hata wanajua haya?— na Kitabu cha Enoki.
VITABU VYA BIBILIA VILIVYOPOTEA
Ninawaonya! Msithubutu kumguza huyu aliye na upako — msithubutu kuwaguza hawa wana na binti zangu walio na upako. Ni heri mzibe midomo yenu.
Mtajua yupi ni nabii bandia. Hawatawaongoza kuenda Mbinguni. Hawatawaambia mtubu. Hawatawaambia kukemea shetani. Hawatawafunza vile vya kufanya vivi hivi. Hawatatabiri yajayo. Watatumia tu habari ambazo yeyote anaweza kutumia.
Nitayasema haya tena. Msiguze Huduma hii! Kwa kuwa kwa uwazi na uvumilivu husema — na Elisheva hata haruhusiwi kuwa katika video kwa hivyo msifikirie au kumwangalia yeye ni kama ni MUNGU kwa sababu yeye huzungumza Maneno ya MUNGU; yeye ameokolewa na Damu, Damu ile ile ambayo pia [iliwaokoa] nyinyi.
Na Nimewatenga yeye na Ezra kufanya Misheni na kazi ambazo Nimewakadiri na Nimewateua kufanya, kama Nilivyowateua nyinyi kufanya.
Lakini lazima iwe ni nyinyi mnaonitafuta MIMI kujua haya: Je, Ni kwa nini nilizaliwa duniani humu? Ni vipi ninavyoweza kukusaidia WEWE? Ni vipi ninavyoweza kukufariji WEWE? Ni nini unachotaka MIMI kusema? Ni nini unachotaka MIMI nifanye?
Msitarajie kuwa Nabii huyu atakuwa na jibu lenu. Wakati mwingine Nitamwambia, lakini hawawezi kujibu maelfu juu ya maelfu ya barua pepe. Hawawezi kujibu maelfu juu ya maelfu, ndio hata Ninaweza kusema mamilioni ya barua, ya simu na mawasiliano. Hawawezi hata kuzungumza lugha yenu. Lazima wategemee wengine kutafsiri lugha hizi.
O maadui, enyi mliolaumiwa, ni nyinyi ndio Ninaowachukia! Na mnasema, “O lakini WEWE hufai kutuchukia sisi!” Lakini si Daudi alisema, ‘Je, Si ninafaa kuwachukia wao ambao wanakuchukia? Ndio Ninafaa kuwachukia na chuki kamili’ (Zaburi 139:21). Chuki kamili ni nini? Ni hawa ambao Ninaowaita waliolaumiwa — Yeremia 6, isomeni!
Zaburi 139:21-22
21Ee BWANA, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako?
22Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu.
Yeremia 6:28-30
28Wote ni waasi sugu, wakienda huko na huko kusengenya. Wao ni shaba na chuma, wote wanatenda kwa upotovu. 29Mivuo inavuma kwa nguvu, kinachoungua kwa huo moto ni risasi,
lakini pamoja na kusafisha kote huku ni
bure, waovu hawaondolewi. 30Wanaitwa fedha iliyokataliwa, kwa sababu BWANA amewakataa.’’
Hadithi ya Bikira 5 wenye Hekima! Isomeni!
(Ona Mathayo 25.) Kuna tu Bikira 5 wenye Hekima na Simaanishi kuwa ni 5 tu — Ninamaanisha wale ambao wanatii kwa kweli.
Na kunao waombezi wanaoitwa “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA” Niliwatuma Malaika Watakatifu kwake kibinafsi, na macho yake aliona mabawa. Aliguza manyoya. Alisikia maneno. Na Nilimpa jina hilo! Na ole kwa yeyote waliokuwa sehemu ya kikundi hiki cha waombezi Niliowaamini — lakini Nilijua, kama Yudasi itakuwa tu kwa muda na wakawasaliti [Huduma hii] kwa kuwa hawakuweza kukubali kiwango cha Maisha na Utakatifu.
Tazameni haya na Nimewaambia siri hii: Wakati Moshe (Musa) alipoenda juu ya Mlima Sinai kwa Amri 10, Sheria 10 ambayo MIMI, YAHUVEH, Niliandika na kidole CHANGU cha moto na kuwaza haya naye Nilipomfunza mengi. Nilimsikiza akizungumza na Nikayasikia maswali yake na yalikuwa mengi. Na alizungumza NAMI na akaniuliza MIMI maswali, yalikuwa mengi.
O lakini watoto wa Israeli ambao Nilikuwa Nimewatoa kutoka kwa utumwa wa Misri, hawakuweza kumngoja arudi. Na wakamuuliza Haruni, “Je, yuko wapi? Hatarudi, kwa hivyo sisi tutaenda kutengeneza miungu yetu.” Na wakachukua dhahabu na fedha, na wakachukua johari na mawe ya thamani (gems), na wakatengeneza sanamu ya dhahabu yenye umbo la ndama kuiabudu na wakaanguka mbele yake. Na wakaabudu kitu ambacho wanaweza kuona na aina zote za tabia mbaya zilifanyika kutoka ushoga hadi usherati, mpaka dhambi zote ambazo sio lazima Nizitaje, hadi wakati Musa aliposhuka na haya ndiyo aliyoyaona. (ona Kutoka 32)
Na Ezra na Elisheva mmeshangaa ni kwa nini kuna wale ambao walijiunga na YDS, “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA” waombezi, waliokuja na kuishi nawe lakini hawakuweza kustahimili kiwango cha Utakatifu ambao unatakikana kuwa Bibi arusi wa YAHUSHUA, wale Bikira 5 wenye Hekima (ona baadaye, Mathayo 24). Lakini sasa mnaelewa Nilivyowapa Neno la kibinafsi kwenu leo na Nikawaambia msilie tena wala kuhuzunika wanapowaacha na kubadilika kuwa adui au wanaenda zao polepole.
Sasa mnapaswa kuwatazama na msihuzunike tena. Na mnapaswa kukumbuka waligeuka yale Niliyowafunza. Kwa kuwa wote walijua Unabii zote ni kweli, hata wale walioenda. Na kuna mtu aliyeitwa kiongozi hapo awali, kabla Ezra, aliwaambia siku moja — na katika siku ya kuadhimisha miaka 14 [ya ndoa] na wajua kuwa imepita miaka 7 [kuwa] yeye alikataa kufanya Nilichomwambia afanye. Yeye hakuwahi kuwa kiongozi.
Hakujawahi kuwa na kiongozi katika Huduma hii ila mmoja na ni mpaka Ezra alipokuja. Sasa kunaye kiongozi wa kiume. Hapo awali, ilikuwa wewe tu. Hapo awali, ilikuwa wewe Elisheva tu. Hakukuwahi kuwa na kiongozi mwingine ila mmoja na ilikuwa wewe Elisheva uliyesikia maagizo YANGU kutoka Mbinguni na ulitii.
Lakini sasa Ninaleta Yuda na Efraimu pamoja (Ezekieli 37:19). Na Ninataka msherehekee haya siku ya Shavuot. Nimewaletea Nabii Mwisraeli, Ezra, na Huduma hii imeenda njia tofauti Ninapowafunza zaidi, njia za Kiyahudi, kama Yuda na Efraimu walivyoolewa pamoja.
Ezekieli 37:19-21
19Waambie, “Hili ndilo YAHUVEH MWENYEZI asemalo: Nitaichukua fimbo ya Yosefu, iliyoko mikononi mwa Efraimu na ya makabila ya Israeli yanayofungamana naye na kuiunganisha na fimbo ya Yuda, nikizifanya kuwa fimbo moja, nao watakuwa wamoja katika mkono wangu.’ 20Inua mbele ya macho yao zile fimbo ulizoziandika 21kisha waambie, ‘Hili ndilo YAHUVEH MWENYEZI asemalo: Nitawatoa Waisraeli katika mataifa walikokuwa wamekwenda. Nitawakusanya po pote walipo na kuwarudisha katika nchi yao wenyewe.
Hakuna kati yao wawili ambaye atawahi kuwafunza kutenda dhambi. Watakapowafunza kutenda dhambi, hapo ndipo mnafaa kukimbia. Hawatawahi kuwaambia kutazama mungu mwingine ila tu UTATU TAKATIFU. Hawatawahi kuwafunza kuyaacha Maandiko Matakatifu, alafu wawaambie kuwa kuna MASIHI mwingine. Kwa kuwa Nimewawekea upako kusema tu ukweli.
Kwa hivyo tena Ninasema vita imekadiriwa kutoka Mbinguni, kutoka kwa MIMI YAHUVEH. Kwa wale wote walioandika maneno yao ambayo yamekaa hapa Mtandaoni, na yamejaa uongo na kashfa, nyinyi ni waliolaumiwa katika macho YANGU! Mtawekwa pale ambapo malaika walioanguka wamewekwa pale ambapo Enoki anavyoita Mbingu ya 3, 18lakini mwaijua kama jehanamu. Na mateso yenu itakuwa hata zaidi ya malaika walioanguka kwa wale waliofanya haya.
Hamkuwahi kutubu hata ingawa mlijua Ninazungumza Ukweli kupitia kwake. Mlifanya mpango na shetani na mmekataa kuutoka. Na mtalipa gharama kwa kila chozi ambalo lililomwagika mlipoumiza uongozi huu na wale wanaohudumu kando yake.
Kwa kila wakati ulipokashifu na kusema uongo juu ya majina yao, kwa kila chozi lililomwagika, Nimeiongeza sasa mara milioni — kama tena Ninavyongoja na Nimewaambia wasitoe Neno hili hadi siku ya Shavu’ot — nyinyi ambao mlikejeli Ndimi Takatifu, Nitawaonyesha vile Nitakavyowakejeli wakati kila kitu kitakapochukuliwa. Kwa kuwa nyinyi nyote mliolaumiwa na nyinyi nyote mnaokataa kutubu, sikizeni haya. Nendeni mkasome Kumbukumbu la Torati 28, laana za MIMI YAHUVEH! Kwa kuwa mtavuna kila moja yake!
Na nyinyi nyote mnaojitahidi kutii na kuabudu YAHUSHUA na MIMI YAHUVEH na IMMAYAH RUACH HA KODESH MPENDWA, ROHO MTAKATIFU, someni Kumbukumbu la Torati 28, baraka Nilizowahifadhia nyinyi wanaojitahidi kutii kila neno Ninalosema.
Kwa nini Niseme, “Kueni Watakatifu kama MIMI Nilivyo Mtakatifu,” (1 Petro 1:16 nk) kama hakungekuwa na kitu kama Utakatifu? Ni kwa sababu Niliweka RUACH HA KODESH ndani yenu kwa hivyo mnajua lililo sawa kutoka kwa lisilo sawa na mnajua mnapotubu dhambi na wakati hamtubu dhambi.
Msifikirie kuwa nyinyi hutenda dhambi kila siku. Kwa kuwa Ninaposema wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa YAH, (Warumi 3:23) inamaanisha kuwa wakati fulani katika maisha yenu mlikuwa mmeyafanya haya kabla hamjampa YAHUSHUA maisha yenu. Lakini hakuna yeyote, hakuna yeyote, hakuna yeyote ambaye kwa kweli ni wa YAHUSHUA atakayepanga kutenda dhambi maksudi (1 Yohana 5:16-17), atakayepanga mbele [ya wakati] kuona ni mpaka wapi wanaweza kuegemea juu ya jehanamu kabla hawajaanguka ndani.
1 Yohana 5:16-18
16Kama mtu akimwona ndugu yake anatenda dhambi isiyo ya mauti, inampasa aombe, naye MUNGU atampa uzima mtu huyo, yaani, kwa wale ambao dhambi yao si ya mauti. Iko dhambi ya mauti, sisemi kwamba utaomba kwa ajili ya hiyo. 17Jambo lo lote lisilo la haki ni dhambi, lakini iko dhambi isiyo ya mauti. 18Tunajua ya kuwa yeye aliyezaliwa na Mungu hatendi dhambi, [yaani, hapangi kutenda dhambi].
Haya ndiyo Maneno ya Faraja Niliyo nayo kwenu mnapochukua wakati kunifariji MIMI.
Tulilie SISI UTATU TAKATIFU. Mwaona SISI hatukutaka — na jehanamu haikutengenezwa kwa binadamu. SISI hatukutaka mtende dhambi. SISI hatukutaka nyinyi kuasi kule Mbinguni. Mlikuwa tayari mmefanya maamuzi hayo, ni upande wa nani utapigania, kama itakuwa MIMI YAHUVEH au shetani. Na sasa kila mmoja anatimiza wokovu wake mwenyewe kwa kuogopa na kutetemeka (Wafilipi 2:12). Kwa kuwa nafsi yako tayari inajua mahali itakapoenda.
Lakini hakuna yeyote aliye mlaumiwa kama bado wanayo hamu — na hata kuyasikia Maneno haya sasa na kujua kwamba ni ya Kweli. Tubuni. Ombeni msamaha kwake YAHUSHUA. Ulizeni mwanzo mpya na dhambi zenu zitakuwa mbali nanyi kama Mashariki ilivyo mbali na Magharibi.
Kwa kuwa kuna dhambi moja ambayo haiwezi kusamehewa kamwe na hili ni kufuru [ROHO MTAKATIFU] (Mathayo 12:31 nk). Lakini kumbukeni mnapoita yale ambayo ni mazuri maovu, (Isaya 5:20), pia mpo hatarini kwa nafsi yenu kwa kuwa hamjamtusi mtu huyo. Mmemtusi MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH. Kuna ufafanuzi tofauti ya neno kufuru, kwa hivyo tubuni kama bado kuna nafasi.
Isaya 5:20
20Ole wao wanaoita ubaya ni wema na wema ni ubaya, wawekao giza badala ya nuru na nuru badala ya giza, wawekao uchungu badala ya utamu na utamu badala ya uchungu!
Tufariji SISI. Je, mwafikiria kuwa SISI huhisi vipi tukijua kuwa mmoja anayesema anatupenda SISI kutoka mwanzo, anapokea Huduma hii, anapokea Unabii hizi katika upendo, na kuwashukuru kuwaongoza kwake YAHUSHUA. Ni barua pepe ngapi zinazokuja na ni mara ngapi imesemwa, “Asante, asante kwa kutuongoza na kutufunza sisi kuwa kuavya mimba ni dhambi, ushoga ni dhambi” (kwa sababu makanisa yenu hayatahubiri Utakatifu ni nini tena) alafu unaanguka. Na hauanguki haraka. Unaanguka polepole kama uasi na matamanio yako kuishi maisha yako inakuingia. Na siku moja unafungua macho yako na kutambua kuwa umeanguka mbali na Neema. Ulianguka mbali na Huruma. Sasa yale yaliyobaki ni mlaumiwa.
Mtawajibika kwa yale mnayoyajua. (Mathayo 12:36)
Kwa hivyo Nimewapa Elisheva na Ezra maagizo. Elisheva hafai kumwaga chozi lingine kwa mwingine anayeita “mtoto” [lakini alianguka].
Kwa kuwa waona na Ninazungumza kwa wote walio kote duniani sasa, nyinyi sio tu kongamano kwao. Mnapopokea ukweli za Huduma hii na Unabii, wameambiwa kuwaita nyinyi “watoto.” Na wanawaombea nyinyi kama watoto. Na Elisheva amepewa moyo wa IMMAYAH. Na Ezra WANGU, yeye ni kama Musa Mpya na yeye ni kama Eliya Mpya. Kwa hivyo jihadharini mnapowakosea.
Lakini jueni kuwa mnapotuma Baraka — hata kama hawawezi kuwajibu au kuwapigia simu, wanaweza tu kuyafanya haya Ninapowaambia — wao husoma baraka hizi na wanazituma baraka hizo kwenu.
Na “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA”, wale waaminifu wa kweli, Elisheva na Ezra hata hawajui majina yenu yote kwa kuwa mmetawanyika kote duniani. Na kunao 500,000 ambao wamekusanyika kwenye ukuta. Ni ukuta wa kiroho kwa kuwa Huduma hii ni Hekalu bila kuta kwa kuwa inajumuisha dunia sasa katika lugha zaidi ya 45 ambayo wanajua.
Lakini imeenea kwa maneno mdomoni na hata wanapozungumza katika ndimi kwa wale Watakatifu [watakatifu, waumini], hata hawajui kuwa wanainua majina ya hawa wawili. Na Ninawaambia sikilizeni, sikilizeni, sikilizeni, sikilizeni na mniulize MIMI wao ni nani. Na kwa wale Watakatifu [watakatifu, waumini wanaoishi kwa Utakatifu], Nitawaambia Ukweli. Na mtafurahia watakapotuma baraka kwenu.
Haya ndiyo Maneno ya faraja ambayo Ninayo kwenu.
Ninapolia, Tunapolia, UTATU TAKATIFU, na SISI Tunawalilia kila mmoja anayeanguka hata ingawa SISI Tunajua kuwa mtaanguka na kukosa kuinuka tena na jehanamu itakuwa nyumbani kwenu — SISI bado Tuliwaumba nyinyi na kama mtoto Tuliwapenda mpaka mlipogeuka kuwa walaumiwa.
Na kwa wale Wageni, kumbukeni wote wamebarikiwa walioalikwa kwenye Karamu ya Arusi ya MWANA-KONDOO (Ufunuo 19:9). Bibi arusi ni 288,000 (Ufunuo 14 na 7) na Tunawatenga na yote yanahusika na kutii. Je, utatii? Au utageuka? Je, utakuwa vuguvugu na kufikiria bado utaenda Mbinguni?
Kumbukeni tena mfano wa Bikira 5. Kumbukeni kuwa kulikuwa na Wapumbavu [bikira] pale, lakini kulikuwa na kikundi kingine (Mathayo 25:11-12) ambao huwa hutajwa nadra sana: na ni wale waliogonga mlango wa BWANA ARUSI baada ya YAHUSHUA kuingia chumbani na Akafunga mlango. Na wakaugonga mlango na kusema, “Turuhusu kuingia” kama walivyofanya kwa Safina ya Noa na akasema, “Nendeni nyinyi wafanyikazi wa maovu kwa kuwa sijawahi kuwajua.”
HADITHI YA BIKIRA KUMI
MATHAYO 24
BIKIRA KUMI: 5 WENYE BUSARA NA 5 WAPUMBAVU
25“Wakati huo, Ufalme wa Mbinguni utakuwa kama wanawali kumi waliochukua taa zao na kwenda kumlaki bwana arusi. 2Watano wao walikuwa wapumbavu na watano walikuwa wenye busara. 3Wale wapumbavu walichukua taa zao lakini hawakuchukua mafuta ya akiba, 4lakini wale wenye busara walichukua taa zao na mafuta ya akiba kwenye vyombo. 5Bwana arusi alipokawia kuja wale wanawali wote wakasinzia na kulala.
6“Usiku wa manane pakawa na kelele: ‘Tazameni, huyu hapa bwana arusi! Tokeni nje mkamlaki!’ 7“Ndipo wale wanawali wote wakaamka na kuzitengeneza taa zao. 8Wale wapumbavu wakawaambia wale wenye busara, ‘Tupatieni mafuta yenu kidogo, taa zetu zinazimika.’ 9“Lakini wale wenye busara wakawajibu, ‘Sivyo, hayatutoshi sisi na ninyi pia. Afadhali mwende kwa wauzao mkajinunulie mafuta yenu. 10“Nao walipokuwa wakienda kununua mafuta, bwana arusi akafika. Wale wanawali waliokuwa tayari, wakaingia ndani pamoja naye kwenye karamu ya arusi na mlango ukafungwa.
WALE BIKIRA WENGINE
11“Baadaye wale wanawali wengine nao wakaja, wakaita, ‘Bwana! Bwana! Tufungulie mlango!’ 12“Lakini yeye bwana arusi akawajibu, ‘Amin, amin nawaambia, siwajui ninyi!’
13“Kwa hiyo kesheni, kwa sababu hamjui siku wala saa ambapo BEN ADAM [MWANA WA ADAMU [MWANA WA YAH] arudi.’’
Hakikisha kuwa umejua kwa kweli MUNGU BABA NI NANI na MWANA WA MUNGU na MUNGU ROHO MTAKATIFU, kwa wote WATATU ni MOJA, hakikisha unajua nani kwa kweli ingawa SISI sote ni tofauti bado SISI Tunakubaliana kamwe na kamwe SISI ni MOJA.
Na hawa ndio walaumiwa wanaogonga mlangoni. Hawa ndio wale ambao hawatawahi kupata msamaha.
O huzunikeni kwa binafsi YETU! Tulilieni SISI! Tufariji SISI!
Niliwapa dunia nzuri. Sasa anga imejaa sumu. Maji ni sumu. Chakula ni sumu. Ombeeni kila kitu. Msidharau chochote. Hata nguo mlizovaa — hamjui kuwa — kemikali zimewekwa pale kuwaua!
Sasa viongozi wa dunia hii ya maovu wa shetani (Waefeso 6:12 nk) — Adamu alipoanguka dunia hii ilianguka katika mkono wa shetani, na matajiri wa kishetani, illuminati iliinuka na sasa wote wanasema, “Lazima tuue. Idadi ya watu ni kuu sana.” Na kwa hivyo wanatia sumu angani na haya huitwa “chemtrails” na inafaa kuleta vipigo.
Ndio sababu Niliwaambia kujifunza Zaburi 91 kama Nilivyomwambia Elisheva mwaka wa 2001. Rudia kila siku. Idai. Simama juu yake na pia Zaburi 23, ishikilie. Msiiachilie! Na mkizidi kutafuta njia ya kutufariji SISI Tunapoona kile walichofanyia dunia hii — Tunavyoona kile Monsanto walichofanya, Tunavyoona sasa wanatengeneza hata johari na vipande vya watoto waliotolewa tumboni na hamyajui haya. Mnafikiria kuwa mnapaka cream kwenye nyuso zenu kurejesha ujana. Hamyajui haya na pale, kuna damu ya DNA.
O Watoto WANGU! Watoto WANGU! Watoto WANGU! Kuna tu njia mbili ya kutoka dunia hii! Ni heri mpige magoti sasa hivi kabla wakati haujaisha!
Ninawaambia haya, sasa Wokovu ni bure lakini kama wewe sio Bibi arusi wale 288,000 (Ufunuo 7 na Ufunuo 14) — na [Bibi arusi wa] Ufunuo 14, Ninawaambia haya, nyinyi mtaenda mbele [ya Bibi arusi wa] Ufunuo 7. Na kuna siri nyingine ambayo Nitaitoa sasa kuwa Elisheva na Ezra na “Wakanyaga pepo wa YAHUSHUA” wanajua, kuna kitu kimoja kingine lazima kifanyike. Na Sizungumzi juu ya mambo ya dunia hii. Ninazungumza ufunuo wa Mbinguni, zawadi Niliyowapa Ezra na Elisheva, lakini bado wapo katika Ufunuo 14 — Kwa wale wengine Ninasema: Kama hauwezi kuyafanya haya sasa ikiwa bure, je, utafanya nini wakati wa Dhiki Kuu?
Je, utanikubali MIMI vipi katika Dhiki Kuu, MWANA WANGU YAHUSHUA katika Dhiki Kuu utakapoambiwa, “Dini zote ziwe moja”? — wakati tayari ishakuwa vile — Rais tayari ameitia saini katika amri yale ambayo sikutaka ifanyike. Kwa kila dini na wale wanaoabudu miungu mingine, wasioabudu MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH.
Dini zote haziwezi kuungana pamoja kamwe na mtarajie kupatikana Mbinguni — wasipotubu na kuacha miungu bandia — hawajafanya chochote ila tu kutengeneza sanamu ya dhahabu ya mfano wa ndama kama vile wakati wa Musa (Moshe) pale Mlimani Sinai ambayo tayari Nishawapa hadithi yake.
SISI Tunahitaji kufarijiwa. SISI Tunataka kujulikana kuwa Tunapendwa. SISI Tunahitaji kusikia kuwa Tunathaminiwa. SISI Tunahitaji kujua kuwa mnajali wakati watoto wanapotolewa tumboni mwa mama zao na kutupwa kama takataka na viungo vyao kuuzwa na wanararuliwa kama bado wako hai.
Je, mwafikiria kuwa SISI hatulii wakati watu wa kishetani wanafanya ibada za kishetani na kuwatesa na kuwalawiti — hata [kwa] watoto wachanga — inapofanyika? Je, kuna chochote kingine kizuri kama mtoto mchanga au mtoto? Lakini mnasimama pale na kutofanya chochote! Mnaogopa hata kuunga maandamano ya kupinga na kusema, “Tunafaa kulinda watoto wetu! Hatufai kuua watoto wetu!”
Je, ni wangapi kati yenu ambao mpo katika maandamano haya kama vile wanaume hawa hawaogopi hata kuyaweka maisha yao chini au hata kuwekwa jela? Nyinyi ni waoga katika Macho YANGU na pale Kitini cha Enzi cha Hukumu mtasikia na mtajua yale ambayo Nitakuwa nayo ya kusema Nitakapowaambia, “Nendeni nyinyi wafanyikazi wa maovu” kwa kuwa hamkujali kamwe mliposikia maovu haya Ninayoita pedophiles.
Hamjui, hamwelewi. Mnafikiria kuwa mnaweza epuka kwa kukataa ukweli lakini hamtafanya hivyo baada ya kusoma haya! Hapana, hamtafanya hivyo baada ya kusoma haya! Kwa kuwa mtawajibika (Mathayo 12:36)!
Je, mnafanya nini kuwasaidia? Ni vipi na — mnafanya nini kuwatia moyo wale wanaoweka maisha yao chini kusema, “Kuavya mimba sio sawa, kuavya mimba ni dhambi, kuavya mimba ni kuua!”
Hamwezi kutenda usherati na watoto na kufikiria kuwa MIMI MUUMBA YAHUVEH Nimefunga macho YANGU na Nimeziba Masikio YANGU na kuufunga Mdomo WANGU kwa kilio na kelele za wale watoto wadogo wasio na hatia.
O mtaona! Katika ulimwengu huu, mnadhani kuwa mko huru kutenda maovu haya na Ninazungumza na nyinyi mnaojiita “baba”! Nyinyi sio baba! Nyinyi ni mbegu ya kibiolojia tu iliyofanywa kuungana na yai ili kutengeneza mtoto, lakini nyinyi sio baba!
Nyinyi ambao mnawaumiza watoto! (Mathayo 19:6; Marko 9:42)
Marko 9:42
Kama mtu ye yote akimsababisha mmojawapo wa wadogo hawa wanaoniamini kutenda dhambi, ingekuwa afadhali mtu huyo afungiwe shingoni mwake jiwe kubwa la kusagia na kutoswa baharini.
Na nyinyi matajiri wa kishetani mnaofikiria kuwa hii ni burudani na mmefanya kila dhambi ambayo inawezekana kufanywa. Kwa hivyo mnajipendekeza zaidi kwake shetani na kusema, “Ni nini kingine ninachoweza kufanya kukutumikia?” Kwa hivyo hata anapowaambia kurarua mtoto katika vipande viwili, na mikono yako mtajaribu kuing’oa mikono yao! Mtavunja vidole vyao! Mtakunywa damu yao! Mtajipaka kwenye nyuso zenu na kuiita “cream ya uso”.
Hamjui ni nini iliyoko kwenye cream hiyo! Hamjui iliyoko kwenye lipstick hiyo! Hamjui ni nini walichofanya — ni hao tu matajiri wa kishetani wanapowacheka.
Hata wale wanaofikiria kuwa wamezungumza dhidi ya maovu haya, lazima muombee kila kitu mnachotumia ulimwenguni humu!
Hamjui ni nini iliyoko angani ambayo tayari imefichwa kutoka kwa macho yenu. Yale tu mnayoweza kuona ni laini nyeupe lakini hamjui ni nini kinachoshuka chini. Nitawaambia ni nini kinachoshuka chini, lakini haitakuwa sasa hivi siku hii ya Shavuot. Bado sio kwa wakati huu. Nitawaambia haya. Sio katika siku hii, katika Unabii huu, lakini yaja. Na hata Nabii huyu atabahatisha kwa kuwa anajua ni nani anayethibiti Mtandaoni.
Watoto, wale Ninaowaita Watoto WANGU, chukua Neno LANGU kwa uzito, [kupigana na
pedophilia]. (Marko 9:42)
Nyinyi mliofanya haya, ibada ya mateso, dhabihu za kishetani ya watoto na usherati na ulawiti, mtawekwa kwenye sehemu ya jehanamu kama vile Kitabu cha Enoki kinavyosema na malaika walioanguka. Na wale waliofikiria wao ni wakubwa na wenye nguvu na hapo awali walikuwa vivyo hivyo na sasa inasema katika Kitabu cha Enoki, wanapiga kelele kwa kuteswa. Hapa ndipo mtakapoenda.
Kwa hivyo mnafikiria kuwa mnaweza kuepuka adhabu ya kuua. Na mnajua ni akina nani Ninaowazungumzia, enyi wanasiasa. Mpo katika Congress. Mpo katika Seneti. Mpo katika mifumo ya Mahakama. Mmekuwa hata marais na Ninazungumza na Marekani sasa. Na bado sitaacha hapo. Ninazungumza na Uingereza.
Ninazungumza na kila [taifa] kote duniani. Mnajua, na watu watajua, hao ni nani.
Ninajaribu kufanya ndimi ziwe fupi sasa, ili msipoteze hamu. Ninavyojenga ujasiri ndani ya mtoto WANGU, Nabii huyu, Mtume huyu, Ringmaiden WANGU, lakini Ninataka kuzungumza kwa uwazi.
Hata kwa nyinyi mnaojiita Bibi arusi wa YAHUSHUA, ni heri muombe kuwa mtastahili kuhesabiwa kuitwa Bibi arusi wa YAHUSHUA mpaka mtakapofika Mbinguni kwa kweli. Kwa kuwa kuna mitego nyingi ambayo shetani ameiweka. Na ni wangapi tayari wameanguka ndani yake?
Kwa hivyo tufariji SISI! Tuulize SISI, tunaweza kuwafanyia NYINYI nini ewe BABA WA MBINGUNI?
Je, mnajua haya? Neno linasema haya — na hii ni Bibilia —kuwa mawe yatalia na kunisifu MIMI ikiwa hamtanisifu MIMI. (Luka 19:40)
Je, mnajua haya? Niwaambie siri.
YAHUSHUA Atakapokuja katika UTUKUFU WAKE wote — na Sizungumzi juu ya Kuja KWAKE kwa Kwanza, Sizungumzi juu ya wakati utakapofika wa kuwachukua, [kuwanyakua] — Ninazungumza wakati ambapo dunia mzima itapata kujua, [wakati] waliolaumiwa wamelia. Watalia kwa milima kuwaangukia na kuwaficha kutoka KWAKE — MIMI YAHUVEH — ANAYEKAA KWENYE KITI CHA ENZI na kutoka kwa Ghadhabu ya MWANA-KONDOO AMBAYE NI YAHUSHUA (Ufunuo 6:16)!
Mwaona, ni wakati mmoja tu YAHUSHUA Alisulubiwa! Ni wakati mmoja tu YEYE Aliposema, “BABA wasamehe” kwa kuwa hawajui wanachofanya. (Luka 23:34) Ni wakati mmoja tu — hadi utubu — ndipo Atakapokuulizia msamaha.
O lakini YAHUSHUA Atakapokuja na wote wataona — Ninawaambia siri hii — kutakuwa na symphony. Kutakuwa na muziki mzuri wa ajabu ambao dunia mzima itausikia.
Haya ndiyo nyinyi WANGU wa Mbinguni, mnayosikia sasa, mliooshwa katika DAMU YA YAHUSHUA ILIYOMWAGIKA, mnaoomba katika JINA LA YAHUSHUA, mnaoiishi kwa JINA LA YAHUSHUA, mlioweka maisha yenu chini na kusema, “Ishi maisha YAKO kunipitia mimi — isiwe mapenzi yangu yatakayofanyika lakini mapenzi YAKO ifanyike, isiwe maneno yangu itakayozungumzwa lakini Maneno YAKO izungumzwe.”
Ninazungumza siri kwenu — kwa Ezra, mpendwa WANGU Ezra, unakuja KWANGU kama mtoto na ‘unanifurahisha MIMI sana’ unaposema, na Ninakuuliza haya kupitia huu mdomo wa Elisheva na Ninasema, “Je, Ezra unataka kujua siri?” Na o Ninavyofurahishwa nawe, IMMAYAH hucheka na kutabasamu, YAHUSHUA hutabasamu na nuru Machoni MWAKE unaposema, “Ndio, ndio! Tuambie siri.”
Kutakuwa na nyimbo na itakuwa kile ambacho viumbe wanachongoja. Kwa kuwa wanalia kwa uchungu na hamyajui haya (Warumi 8: 19-23) — uharibifu, uharibifu waja wa yale ambayo yalikuwemo ulimwenguni humu na tena hayamo kamwe lakini yatakuwa tena mara nyingine.
Na viumbe — na udhihirisho, zitakuwa pale: udhihirisho za wana wa YAH na haya yanajumuisha mabinti. Watasaidia haya kutendeka. Kwa kuwa wanalia na kusema — viumbe vyote wanalia na wanangoja na kusema (Warumi 8:19-23) — na Ninazumgumza tena juu ya viumbe wa ulimwengu huu. Wanangoja na wanangoja na wanangoja. Na ni kama vile tu Bibi arusi wanavyongoja kwa udhihirisho wa wana wa YAH na wanangoja na Ninawaambia haya, mtasikia nyimbo, ambayo itakuwa viumbe vyote watakaokuwa wananiimbia MIMI.
Wataimba tu kama ndege wanavyoimba nyimbo za kunisifu MIMI kila asubuhi, hata ingawa zile sumu wanazoziita — chemtrails zilizopangiwa kuwaua na bado Nitawatia fadhaa hao wanasayansi. Na wale ambao kwa kweli ni WANGU na kusimama katika Zaburi 91, haitawaathiri kwa haraka kama vile itakavyowaathiri wengine. Nitawalinda. Nitawalinda kama mtakumbuka kuomba, na kujipaka DAMU YA YAHUSHUA mnapoenda nje.
Lakini Ninawaambia haya. Nisikilizeni MIMI sasa.
Je, waweza kuona akilini simba akinguruma? Je, waweza kumwona simba marara? Je, waweza kuona sio tu ndege wakiimba lakini waweza kuona chura wakikoroma? Je, waweza kuona nyenje akilia? Je, wajua kila mnyama hapo awali alikuwa na sauti? Kila sauti za wanyama na kila sauti za nyenje ambazo — kila sauti — hata ya, hata ya nyuki, wataimba wimbo KWANGU kama vile kwenye Bustani ya Edeni kabla haijaanguka.
Ninawaambia haya. Adamu aliweza — alipokuwa anawapa majina, alizungumza na kila mmoja wao na walimjibu. Na sauti hizo zitarudi tena. Je, haya hayawafurahishi o wapendwa? Je, hamtaki kuyasikia haya? Je, hamtaki kujua siri zaidi? Basi Nitii MIMI kwa kuwa hizi tu ni siri ndogo Ninazowapa.
Singeweza kuweka kila kitu katika kitabu kimoja. Kuna vitabu vingi sana na Unabii hizi na Ufunuo hizi mnazozisikia sasa — fikirieni haya, fikirieni haya watoto WANGU — hamwezi hata kuanza kufahamu ni nini Ninacho kinachowangojea, kwa kuwa nyinyi mlioteseka na mnateswa kwa sababu ya JINA LA MWANA WANGU YAHUSHUA.
O watoto WANGU, o watoto WANGU, o watoto WANGU! Ninavyowapenda! Sio tu Bibi arusi WANGU, lakini pia nyinyi mtakaoitwa Wageni kwenye Karamu ya Arusi ya MWANA-KONDOO! Je, mnajua vile Ninavyowapenda? Je, mnaelewa? Ninawataka, kuwakumbatia. Ninataka mkae pajani MWANGU. O wapendwa WANGU, Nisikilizeni MIMI.
Nisikizeni MIMI leo. O, Nisikizeni MIMI leo.
SISI Tunahitaji Mtufariji SISI. SISI Tunahitaji Mtuimbie SISI. SISI Tunahitaji mtuthamini na kutupenda SISI. Msituulize SISI tu, kutuuliza SISI juu ya maombi inayohitajika, lakini Tuulize SISI, “Je, ni nini Mnachotaka Niwafanyie NYINYI leo? Je, ni vipi Ninavyoweza kuwafurahisha NYINYI?”
Je, mnajua jinsi haya yatakavyotubariki SISI? Je, mnafahamu kweli jinsi haya yatakavyotubariki SISI?
Je, mnajua ni kwa nini Niliwaumba? Je, mnajua kuwa ilikuwa kwa ushirika? Je, mnaelewa kuwa Niliuweka udongo pamoja? Nilichukua ubavu kutoka kwa mwanamume na Nikaumba mwanamke. Mnashangaa, “Je, nywele ilifikaje pale?” — huyu ni Elisheva, unacheka na kusema. Na tena unamtazama Ezra na kusema, “Mpendwa, Ninafikiri ni njia ile ile tu ulivyopata nywele zako”,
Na Ezra ukajibu swali:
Ezra: Kitabu cha Siri za Enoki sura ya 30 mstari wa 10, “Na katika siku ya 6 Nilimwamuru HEKIMA WANGU kumuumba binadamu kutoka kwa vitu 7: Moja: mwili wake kutoka kwa udongo; Mbili: damu yake kutoka kwa umande; Tatu: macho yake kutoka kwa jua; Nne: mifupa yake kutoka kwa jiwe; Tano: akili yake kutoka kwa mbio za malaika na kutoka kwa mawingu; Sita: mishipa yake kutoka na nywele zake kutoka kwa nyasi za ulimwengu na saba, nafsi yake kutoka kwa PUMZI YANGU na kutoka kwa ROHO WANGU.”
Elisheva: Na haya yanatoka kwenye Kitabu —
Ezra: Kitabu cha Siri za Enoki.
Elisheva: Na mpendwa ipo katika ukurasa gani?
Ezra: Imetoka katika Sura ya 30 mstari wa 10.
Elisheva: Na tafadhali msiende kuitafuta kwingine. Ipo papa hapa kwenye Huduma hii.
Kitabu Cha Enoki
Kama utaitafuta kwenye maktaba ya Vitabu Vilivyopotea ya ile wanayoita Bibilia ambayo kwa kweli hazijapotea.
Unabii Unaendelea:
Na haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema — jambo moja lingine la mwisho — na ni yaya haya: Ninataka mjue kuwa nyinyi ni watoto WANGU na Ninataka kucheka nanyi. Ninataka mniulize MIMI maswali ambayo mtafikiria ni ya ujinga lakini Ninataka kucheka na Ninataka kuwapa majibu. Ninataka kufurahia na kuwafunza nyinyi. Ninataka kuwapa ufunuo za siri kama Ninavyompa Elisheva na Ezra. Ninafurahia sana kwa wale wanaompenda YAHUSHUA WANGU kwa kweli na wanaojitahidi kwa kweli kutii kila siku. Na wanapotenda dhambi, kwa haraka, wanatubu kwa haraka. Ulizeni msamaha wakati uo huo.
Na haya sio tu kusema ombi rahisi, “Kama nimekukosea leo basi nisamehe tafadhali.” Niambie MIMI ulichofanya, ili Niweze kukusafisha kutokana na dhambi hiyo.
O watoto WANGU katika siku ya Shavu’ot Ninawapa zawadi hii. Na Ninazungumza kwa wazi nanyi sio tu katika ndimi. Ninazungumza wazi ili kila mtu aweze kuelewa.
Ninajua ni akina nani walio watoto WANGU wa kweli na kwa sababu Niliwafinyanga kama Kitabu [cha Enoki] kilisema — Ninawaambia haya, mtakapoona clones na roboti zinazofanana na binadamu: Kumbukeni shetani ana bandia. Lakini anaweza kweli kufanya kile ambacho MUUMBA amesema sasa hivi, ambapo anaweza kufanya uumbaji kama huo? — hawezi — anaweza tu kukupa uigaji wa kioo. Wanaweza kuwafanya mtengenezwe kufanana kama mwingine na wanawaita hawa clones lakini Ninawaambia haya, Ninawacheka na kuwakejeli hawa wanaoitwa [clones], uigaji!
Ninayo mishangao kwenu nyinyi — vile Nitakavyofanya kuwalinda! Wakati nyinyi matajiri waovu mtafikiria kuwa mmeipata — na Ninajua kuwa nyinyi husikiliza Manabii wa kweli na mnajaribu kuiga na mnajaribu kuenda mbele YANGU ili vitu visifanyike. Na mnajaribu kuharakisha wakati kabla haijakuwa kanuni juu ya kanuni na amri juu ya amri (Isaya 28:10). Tayari Ninajua akili zenu. Ninajua ni nini mtakachofanya na tayari Nimeenda mbele yenu!
Na tayari Ninajua vipi Nitakavyofanya kuwalinda Watoto WANGU Wapendwa, Bibi arusi, Wachaguliwa na Wateule!
Na haya ndiyo Maneno ya faraja Ninayowapa.
Sasa mtakapoyasikia haya, kama mtayapokea, basi Nipe MIMI sifa, heshima na utukufu kwa kuwa Nimechukua wakati huu kuzungumza kupitia Ringmaiden WANGU. Na Nimewapa wakati kwa sababu Ninawapenda sana. Ninataka kuwajua zaidi. Ninataka mjifunze kutii.
Ninataka mtii YAHUSHUA na msiwahi kumkana YEYE, hata kama inamaanisha — na Ninazungumza kwa Wageni sasa wa Karamu ya Arusi ya MWANA-KONDOO, hamwezi kufika kipimo cha kuwa Bibi arusi na mnayajua haya, lakini mtii. Jitahidi kutii tu na msiwahi kukana, katika huu Ninaouita Wakati wa Dhiki wa Yakobo (Yeremia 30:7). Kamwe, kamwe msikane JINA LA YAHUSHUA [katika] kile kitakachoitwa Dhiki Kuu, kamwe msikane JINA LAKE hata ingawa itamaanisha maisha yako — hata ingawa inamaanisha kuwa utalazimika kuweka kichwa chako kwenye chuma baridi ya guillotine.
Na utajua kabla hiyo haijakuja chini kwenye kichwa chako, utamlilia YAHUSHUA na roho yako itachukuliwa kabla mwili wako haujauhisi ule kisu.
Na mnaona enyi maadui WANGU, mnaona hawakuwa na, hawatakuwa na utukufu. Kwa kuwa hata haukuuhisi! Badala ya hayo utakuwa unasimama mbele YANGU Mbinguni ukiwa umevaa vazi nyeupe. “O ni akina nani hao waliotoka kwenye Dhiki Kuu wakiwa wamevaa mavazi meupe,” katika nambari kuu isiyoweza kuhesabiwa (Ufunuo 7:13-17)?
Ni nyinyi mtakaoitwa Wageni katika Karamu ya Arusi ya MWANA-KONDOO.
Haya ndiyo Maneno Ninayowafariji nayo. Je, ni maneno gani mtakayonifariji MIMI nayo? Je, mtatii vipi? Je, mtapinga vipi dhidi ya kuavya mimba na maovu yanayofanyika katika dunia hii leo? Je, mtabaki tu kimya? Kwa kuwa wanaume wazuri wanapobaki kimya maovu hushinda. Je, ni wangapi kati yenu walio kimya?
Na makanisa YANGU yako wapi? Je, wapi wale wanaotangaza jina la YESU KRISTO? Je, mbona hamuulizi maswali huyu anayeitwa papa? Je, yuko wapi? Nitawaambia yeye yuko wapi. Hayuko upande wenu.
Lakini lazima mpinge! Lazima mzungumze! Lazima katika njia fulani mfanye kitu kuthibitisha kuwa kwa kweli nyinyi ni WANGU na kumtumikia YAHUSHUA.
Na kumbukeni haya. Hakuna, hakuna, hakuna chochote ambacho ni muhimu sana kukufanya kukosa MIMI YAHUVEH, YAHUSHUA na IMMAYAH, ROHO MTAKATIFU MPENDWA. Lakini hakuna chochote ambacho ni muhimu sana kukufanya ukose Mbinguni! Na o matokeo yale kama utakosa!
SISI Tunataka kufuruhia sana na kukukaribisha! Lakini tena, yote ilikadiriwa hapo mbeleni: kama utasikiliza, kama utatii, kama utatubu na kuja KWAKE YAHUSHUA leo hii.
Na wakati shetani atasema, “Ah ha! Nimekupata katika dhambi leo!” kumbuka Nilisema, lia kwa haraka — katika Jina la YAHUSHUA — sema, “O pole sana Nimefanya haya. Tafadhali nisaidie nisirudie tena.” Na amini kuwa imesamehewa pale Msalabani, kama tu hautaendelea kutenda [dhambi] maksudi, kama tu hautasema, “O sasa nina kisingizio cha kutenda dhambi katika njia zote kwa sababu YAHUSHUA Alilipia gharama pale msalabani kwangu mimi pale Kalivari.” Hii sio sababu haya yalifanywa!
Na mnajua enyi wapumbavu gharama ambayo mtalipa kwa kufunza — na Ninazungumza kwa makanisa za sasa wanaofanya haya —kuwa “hakuna kitu kama dhambi; msijali kuhusu haya tena.” Na mnakataa kuzungumza juu ya Utakatifu. Mnakataa kwa sababu mmenyamaza — [mmenyamazishwa] na serikali.
Lakini hata [Rais] Donald Trump alisema, Na hata [Rais] Donald Trump alipitisha amri kuwa mmeruhusiwa kuzungumza katika uhuru kwa wakati huu. Itumieni kama bado mnaweza. Itumieni kama bado mnaweza kwa kuwa wakati unakuja hivi karibuni na tayari mnaiona kama Youtube inavyonyamazisha na Google inavyonyamazisha na Facebook inavyonyamazisha na kila mtandao — mnafikiria kuwa sijui majina yao? Mnafikiria kuwa sikujua kabla ya wakati kuwa haya yatafanywa?
Tumieni uhuru wenu watoto WANGU kama bado mnaweza. Na Ninazungumza onyo hili kote duniani. Tumieni uhuru huu kama bado mnaweza, katika njia yoyote ambayo mnaweza.
Na haya ndiyo Maneno Ninayo ya kusema katika haya, itakayotolewa katika siku ya, Shavu’ot 2017.
Mwisho wa Neno.
Ezra: Asante BABA YAHUVEH, asante YAHUSHUA, asante IMMAYAH kwa Neno hili la ajabu ambalo umetupa sisi, ufunuo na siri nzuri. Tunabariki JINA LAKO TAKATIFU. Tunakufariji WEWE BABA YAH. Tunakufariji WEWE YAHUSHUA. Tunakufariji WEWE IMMAYAH katika JINA LA YAHUSHUA. Amina.
Elisheva: BABA YAHUVEH, Ninataka kukushukuru. Ninataka kukusifu. Mimi sio tofauti na yeyote kama Ulivyosema. Mimi ni Mjumbe WAKO tu. Wakati mdomo huu unapofunguka, sijui ni nini Utakachosema. Ninajifunza ufunuo pamoja na kila mtu. Mimi sio mmoja ya wale wasomi wapumbavu. Sijifunzi kutoka kwa shule yoyote ya theolojia. Mimi ni mtenda dhambi tu aliyeokolewa kwa neema. Na Ezra nami huishi maisha yetu kila siku ili kuwa na ushahidi kama wa Enoki, kupatikana tunakufurahisha WEWE.
Hili ndilo kilio chetu na kinafaa kuwa kilio cha kila mmoja anayetaka kuwa mmoja wa sehemu ya Bibi arusi wa YAHUSHUA. Ulizeni kuwa na ushahidi kama wa Enoki, kuwa mpatikane kumfurahisha BABA YAHUVEH (Waebrania 11:5-6) na sio lazima kufa na mtanyakuliwa hadi Mbinguni, angani.
Hebrew 11:5-6
5Kwa imani Enoki alitwaliwa [hadi Mbinguni] kutoka katika maisha haya, kiasi kwamba hakuonja mauti. Hakuonekana, kwa sababu MUNGU alikuwa amemchukua. Kwa kuwa kabla hajatwaliwa alikuwa ameshuhudiwa kuwa ni mtu aliyempendeza MUNGU. 6Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza MUNGU, kwa maana ye yote anayemjia MUNGU lazima aamini kwamba YEYE yuko na ya kuwa HUWAPA THAWABU wale wamtafutao kwa bidii.
Mwisho wa Rekodi.
Ilivyozungumzwa, ilivyoandikwa
katika JINA LA YAHUSHUA,
Mei 29, 2017
Mtume, Nabii Elisheva Eliyahu